MENEJA WA UWANJA WA CCM KIRUMBA AHIMIZA USAFI UWANJANI HAPO.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Meneja wa Uwanja wa CCM Kirumba Steven Shija (kushoto) akipokea mifuko ya saruji kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi Mzunguko wa Uwanja huo, Michael Omollo (kulia).
Judith Ferdinand, Mwanza
Meneja wa Uwanja wa CCM Kirumba uliopo wilayani Ilemela jijini Mwanza Steven Shija, amewataka wajasiriamali na mafundi wanaofanya shughuli zao, kwenye maeneo yanayozunguka uwanja huo kufanya usafi ili kuweka mazingira katika hali ya usafi ili kuepukana na magonjwa ya milipuko.
Hayo aliyasema juzi wakati alipokuwa akipokea msadaa wa mifuko ya saruji 35 yenye thamani ya sh 542,500 kutoka kwa wajasiriamali na Mafundi wa mzunguko wa uwanja huo alisema, ili kuweza kufanya kazi kwa amani na salama bila kuugua ni vema kila mtu akafanya usafi katika eneo lake ya kazi.
Shija alisema, ifike wakati kila mtu atambue kuwa tunza mazingira ya kutunze kwani afya yako ndiyo mtaji wako kuzingatia hayo hakuta kuwa na mtu ambaye atafanya shughuli za kujiingizia kipato katika eneo uchafu.
“Nawaomba ndugu zangu mzingatie usafi, ili kuepuka kuugua magonjwa ya mlipuko nimewaruhusu kufanyia hapa kazi nikiwa na lengo kila mtu ajipaitie kipato halali kulingana na kazi zenu,”alisema Shija.
Pia alisema,ni vema kutumia jumamosi ya mwisho ya mwezi iliyotengwa na Raise John Magufuli kama siku ya usafi, kusafisha mazingira yao ili kuwavutia na wateja wao.
Aliwashukuru wajasiliamali hao kwa kujitoa katika kuchangia ujenzi wa miundombinu ya kupitisha maji taka kwa kutoa mifuko ya saruji 35, kwa kufanya hivyo kutasaidia kumalizika kwa ujenzi huo, sambamba na kuhimiza kutrunza mazingira ya eneo hilo ili kuweza kufanya shughuli zao kwa amani.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi wa Mzunguko wa Uwanja wa CCM Kirumba Michael Omollo alisema, kwa kuwa yeye ni kiongozi wa umoja huo ni jukumu lake kuhimiza kufanya usafi katika maeneo ya kazi kwani uchafu adui.
“Tunamshukuru kiongozi huyu kwa kutukumbusha kufanya usafi katika maeneo yetu ya kazi, kwani kila binadamu husahau hivyo kukumbushana ni sehemu ya kazi,”alisema Omollo.
No comments: