LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AHIMIZA MATUMIZI YA EFD's KWA MADEREVA TAX.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

 Na James Salvatory, BMG Dar
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, amewataka wamiliki na madereva tax jijini Dar es salaam kuanza kutumia mfumo wa mashine za kielektroniki (EFD's) kutolea tiketi ambao utakuwa ukionyesha umbali wa safari na nauli husika.

Akizungumza jana wakati wa kikao na wamiliki pamoja na madereva wa tax mkoa hapa, Makonda aliwapa wiki moja kujadili mapendekezo yao ambayo yataweza kuboresha usafiri wa tax kwa jiji la Dar es salaam ikiwa ni pamoja na kutoa tiketi ambazo zitaendana na thamn ya usafiri na kwa kila tax kuhakikisha inakuwa na msitari wa utambulisho

Aidha aliwasisita madereva tax kutoa taarifa za uharifu pindi wazionapo  kwani wao wamekuwa ni watu wa kukutana na watu tofauti tofauti na

Kwa upande wao wamiliki na madereva wa tax wa maeneo tofauti wa jiji Dar es salaam walisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutozwa kodi kubwa na Mamlaka ya Mapato nchini TRA, pia uwepo wa huduma ya Tax kwa njia ya mtandao unafanywa na kampuni ya UBA wameeleza umewaharibia soko kwani kampuni hiyo inatoza bei ndogo zaidi, pia gharama za uendeshaji hazilingani wanajikuta wao wanalipa kodi kubwa zaidi kuliko UBA. 

Katibu Mkuu wa umoja huo, Ramadhani Ashiru alieleza kuwa kampuni hiyo ya UBA inatumia Tax bubu ambazo hazitambuliki kisheria huku kero nyingine ikiwemo uwepo wa bajaji nyingi kinyume na utaratibu, machinga kupanga bidhaa zao barabarani jambo linalowapelekea kutofika kwa wakati maeneo wanayo wapeleka abiria, pia wamewashushia lawama askari wa barabarani kwa kuwaandikia ‘notification’ hata kwa makosa ya kiufundi.

No comments:

Powered by Blogger.