LIVE STREAM ADS

Header Ads

UONGOZI MPYA WA CHAMA CHA SOKA MKOANI ARUSHA WAPANIA KUNYANYUA SOKA MKOANI HUMO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mwenyekiti mpya wa Chama cha Mpira wa miguu mkoa wa Arusha (ARFA) Peter Temu.
Na Woinde Shizza,Arusha
Chama cha soka Mkoa wa Arusha (ARFA) kimefanikiwa kupata uongozi mpya baada ya uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki wilayani Monduli ambao watakaa madarakani kwa miaka minne ijayo.

Katika uchaguzi huo uliokuwa unawaniwa nafasi kumi, ulionekana mgumu kwa nafasi mbili pekee ile ya Mwenyekiti pamoja na nafasi ya Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFFambapo wagombea walikua wawili wawili.

Waliofanikiwa kupita katika uchaguzi huo kwa nafasi ya mwenyekiti ni Peter Temu aliyemshinda Omary Walii kwa kura 13 kwa 6, Katibu mkuu Zakayo Mjema aliyepata kura 18, katibu msaidizi akipita Nassoro Mwarizo.

Nafasi ya Mweka hazina ikienda kwa Omary Nyambuka, Huku nafasi ya Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF Issa Hamisi alimshinda Athumani Mhando kwa kura 13 kwa 8, na nafasi ya kamati tendaji ya ARFA ikienda kwa Soud Abdy.

Washiriki ambao ni wajumbe wa vyama vya soka kutoka Mkoani hapa waliojitokeza ni kutoka Arusha Mjini, Monduli, Arumeru, Karatu, Longido, FRAT ambao walifanya jumla ya wajumbe 19 waliopiga kura.

Huku nafasi ya wajumbe watatu wa kamati tendaji iliyopata mtu mmoja na mwakilishi wa vilabu ambazo hazajajazwa utafayika uchaguzi mdogo baada ya siku 90 kupita alisema katibu wa kamati ya Uchaguzi Seleimani Kirua

Katibu mkuu mpya wa ARFA Zakayo mjema.  alisema wameingia madarani huku kukiwa na deni  kubwa  la  kuitendea haki Arusha ili kuweza kurudisha timu ligi kuu.

"Kwanza nashukuru nimechuguliwa kwa idadi kubwaya kura na hii ni dhahiri wajumbe wameniamini na nitahikisha tunashirikiana kwa pamoja na wilaya zetu katika kuhakikisha soka la mkoa huu linarejea kama ilivyokuwa zamani,"alisema Mjema.

Mwenyekiti mpya Peter Temu aliwasihi wadau wa soka wawe na matumaini kuwa mpira utarejea kulingana na safu mpya yenye morali ya wa kusaidia na kuendeleza mpira.

No comments:

Powered by Blogger.