LIVE STREAM ADS

Header Ads

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA ILEMELA LARIDHIA MACHINGA KUONDOKA MAENEO YASIYO RASMI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, John Wanga (kulia), akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Manispaa hiyo kilichoketi hii leo. Wengine ni Naibu Meya Manispaa ya Ilemela, Shaban Maganga (kushoto) na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Renatus Mulunga (katikati).
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, John Wanga, akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani Manispaa ya Ilemela.
Mstahiki Meya Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga, akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo.
Naibu Meya Manispaa ya Ilemela, Shaban Maganga (kushoto), akiwasilisha mchango wake kwenye kikao cha baraza la madiwani hii leo. Wengine ni Mstahiki Meya Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga (katikati) na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Wanga.
Mbunge wa jimbo la Ilemela Dkt.Angelina Mabula, akiwasilisha hoja zake kwenye kikao cha baraza la madiwani Manispaa ya Ilemela.
Mchumi Manispaa ya Ilemela, Amos Zephania, akiwasilisha taarifa ya mkurugenzi katika katika robo ya pili ya mwaka 2016/17
Afisa Mipango Miji, Manispaa ya Ilemela, Kennedy Chigulu, akijibu baadhi ya hoja za madiwani wa manispaa hiyo.
Diwani wa Kata ya Shibula Manispaa ya Ilemela, Swilla Dede, akichangia hoja kwenye kikao cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo ambapo pia alihoji ni lini zoezi la kuwalipa fidia wakazi wa Mohonze litaanza kutekelezwa ambapo alijibiwa kwamba utekelezaji wa zoezi hilo unashughulikiwa na siku chache zijazo.
Madiwani wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza
Madiwani wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza
Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angelina Mabula (kushoto), akiteta jambo na diwani wa Kata ya Buswelu Manispaa ya Ilemela, Sarah Ng'wani.
Kutoka kushoto ni Kheri James ambaye ni Katibu wa mbunge wa jimbo la Ilemela akiwa na wageni kutoka taasisi ya Wabia Network ya nchini Uingereza ambao ni Steve Martin (katikati) na Judith Martin. Wadau hao kupitia taasisi ya mbunge wa Ilemela, The Angeline Foundation walisaidia ununuzi wa vitabu vya hesabu kwa ajili ya shule za jimboni humo.
Mmoja wa wadau wa elimu kutoka taasisi ya Wabia Network ya Uingereza, akizungumza kwenye kikao hicho baada ya kukaribishwa kusalimia.
Watumishi wa halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Baadhi ya watumishi wa idara mbalimbali Manispaa ya Ilemela.

George Binagi, BMG
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza imewataka machinga wanaofanya biashara zao katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria ikiwemo kwenye hifadhi za barabara kuondoka katika maeneo hayo kwa hiari.

Mkurugenzi wa manispaa hiyo, John Wanga, ameyasema hayo hii leo kwenye kikao cha Baraza la madiwani huku pia akiongeza kwamba zoezi hilo linawahusu wananchi waliojenga katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu.

Ameyataja baadhi ya maeneo ambayo machinga wanapaswa kuondoka kuwa ni pamoja na Ghana, Kona ya Bwiru, Furahisha, Kirumba Sokoni na Kitangiri ambapo machinga katika maeneo hayo wametakiwa kuhamia Soko la Kiloleli ambalo miundombinu yake imekamilika.

Akiwasilisha maazimio ya baraza la Madiwani wa Manispa ya Ilemela, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Renatus Mulunga, amewahimiza wananchi na machinga kutii sheria bila shuruti kwa kuondoka katika maeneo yaliyozuiliwa kisheria ili kuepuka kuondolewa kwa kutumia nguvu ambapo kwa pamoja na mbunge wa jimbo la Ilemela Angelina Mabula wametahadharisha maamuzi hayo kutochukuliwa kisiasa.

No comments:

Powered by Blogger.