LIVE STREAM ADS

Header Ads

KATIBU MKUU WA CCM AONGOZA MAMIA KUMZIKA MNEC WILAYANI SAME.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

 Kaimu katibu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akimpokea Katibu mkuu wa CCM Abdrahman Kinana alipowasili katika mazishi ya Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Marehemu Ally Mbaga wilayani Mwanga  alieyefariki kwa ajali ya gari wakati anatoka katika maadhimisho ya Miaka 40 ya CCM wilayani Rombo, Kilimanjaro.
Katibu Mkuu CCM Abdurahman Kinana aliye valia vazi la kanzu Nyeupe,katibu wa CCM Mkoa wa Kirimanjaro wa kwanza kushoto  pamoja na Kaimu katibu Uvccm Shaka hamdu shaka wakielekea Eneo la Msiba pamoja na makada mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi.
Katibu Mkuu CCM Abdurahman Kinana aliye valia vazi la kanzu  akisalimiana na Kiongozi wa Familiya ya Marehemu Ally Mmbaga.
Katibu Mkuu CCM Abdurahman Kinana aliye valia vazi la kanzu akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick.
"Kwa niaba ya Mwenyekiti  wa CCM Taifa Dk John Pombe Magufuli na  Chama Cha Mapinduzi   nawasilisha kwenu salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa  na wanafamilia yote ya  Ndg Mmbaga  kufuatia msiba huu mzito ambao umewagusa kuwapa huzuni na majonzi  makubwa yasiolelezeka kwa kupoteza nguzo muhimu tuliokuwa  tukishirikiana  katika  mambo mbali mbali"Alisema Katibu Mkuu wakati akiwasilisha salamu  za rambi rambi za  Chama Cha Mapinduzi.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (wa sita kulia) akishiriki kuswalia  jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa NEC, Mwalimu Ali Mbaga wakati wa mazishi yaliyofanyika leo Feb 8, 2017, katika kijiji cha Kighare, Usangi wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro, leo. Mbaga ni miongoni mwa viongozi wanne wa CCM, waliofariki kwa ajali ya gari wakati wakitoka kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya CCM katika mkoa huo.

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana Aliye vaa Vazi la kanzu Katikati pamoja na Viongozi wananchi wakitoka Kuuzika Mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa NEC, Mwalimu Ali Mbaga  aliyezikwa leo katika kijiji cha Kighare, Usangi wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro
 PICHA NA FAHADY SIRAJI  UVCCM

No comments:

Powered by Blogger.