LIVE STREAM ADS

Header Ads

MFUMUKO WA BEI WA MWEZI JANUARI 2017 WAONGEZEKA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, akizungumza jana katika mkutano na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei wa mwezi Januari 2017 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth Minja.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakiwa kazini.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale
MFUMUKO wa Bei wa mwezi Januari 2017 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.8 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.7 ilivyokuwa mwezi Desemba 2016.

Hayo yalibainishwa jana na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakati akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

"Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 105.92 mwezi Januari 2017 kutoka 1-05.04 mwezi Desemba 2016" alisema Kwesigabo.

Alisema kuongeza kwa fahirisi za bei kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula.

Alitaja baadhi za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na mahindi kwa asilimia 6.3, ndizi za kupika kwa asilimia 5.8, magimbi kwa asilimia 5.3 na viazi vitamu kwa asilimia 6.5.

Alisema kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilichochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na mkaa kwa asilimia 3.2 na majokofu kwa asilimia 2.4.

Kwesigabo alisema thamani ya shilingi ya Tanzania hupima badiliko la uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile za mlaji ambazo shilingi ya Tanzania ingeweza kununua katikavipindi tofauti.

"Ikiwa fahirisi za bei za Taifa zinaongezeka, uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma hupungua" alisema Kwesigabo.

Alisema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 94 na senti 42 mwezi Januari, 2017 ikilinganisha na shilingi 95 na senti 20 ilivyokuewa mwezi Desemba 2016.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments:

Powered by Blogger.