LIVE STREAM ADS

Header Ads

MACHINGA JIJINI MWANZA WATUNISHIANA MISULI NA MGAMBO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

#BMGHabari
Vuta nikuvute imeibuka tena Jijini Mwanza katika eneo la Makoroboi baina ya machinga na mgambo wa halmashauri ya Jijini hilo, hali iliyosababisha baadhi ya shughuli ikiwemo maduka kufungwa kwa muda.

Mvutano huo ambao nusra usababishe vurugu kubwa katika eneo hilo la Makoroboi ambalo ni kitovu cha machinga Jijini Mwanza, umetokana na zoezi la kimya kimya la mgambo kuwaondoa machinga katika maeneo yasiyo rasmi licha ya hivi karibuni zoezi la aina hiyo kusitishwa na Rais John Magufuli.

Hatua hiyo imesababisha machinga kutokubaliana na mgambo hao kwa minajiri kwamba walipewa ridhaa ya kusalia katikati ya Jiji na Rais Magufuli hadi watakapoandaliwa maeneo mbadala hivyo yeye ndiye anayepaswa kutoa kauli ya wao kuondolewa katika maeneo wanayofanyia biashara.

Baadhi ya maduka yaliyo jirani na eneo la Makoroboi yamelazimika kufungwa kutokana na mvutano huo kabla ya hali kutulizwa na jeshi la polisi.

Hadi mwanahabari wetu anatoka eneo la tukio, ulinzi wa jeshi la polisi ulikuwa umeimarishwa ikiwemo kufungwa barabara ya Temple inayopita katika eneo hilo la Makorobi.

No comments:

Powered by Blogger.