LIVE STREAM ADS

Header Ads

TIMU YA SOKA YA PAMBA YA JIJINI MWANZA YASHINDWA KUFURUKUTA NYUMBANI MBELE YA LIPULI YA IRINGA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Timu ya Pamba Fc ya mkoani Mwanza imejikuta ikishindwa kufurukuta mbele ya Lipuli Fc ya mkoani Iringa kwa  kuchapwa goli 3- 2, katika mchezo wa lala salama wa msimu wa ligi daraja la kwanza 2016- 2017.

Mchezo huo uliochezwa jana, katika uwanja wa CCM Kirumba  wilayani Ilemela, huku  Pamba wakiwa wenyeji.

Katika mchezo huo Pamba Fc ilifunga goli kupitia washambuliaji  wake James Sungura  na David Julius ,  huku Lupili Fc  wakifunga kupitia washambuliaji wake Zamoyoni Pangapanga, Twalibu Abed na Salum Machako.

Mara baada ya kimalizika kwa mchezo huo Kocha msaidizi wa timu ya Pamba Fc Emmanuel Kingu alisema, wamecheza vizuri lakini wameshindwa kuibuka na ushindi kutokana na kurudia makosa.

Naye Kocha Msaidizi wa Lupili Fc Julio Elieza alisema, licha ya baadhi ya wachezaji kuugua baada ya kufika Mwanza kutokana na hali ya hewa,lakini wamefanikiwa kuibuka na ushindi ugenini.

Hata hivyo  timu ya Lupili Fc  imefanikiwa kufuzu kushiriki ligi kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2017- 2018, huku Pamba Fc ikibaki katika ligi daraja la kwanza msimu wa 2017- 2018.

No comments:

Powered by Blogger.