LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZIRI NAPE NNAUYE AENDELEA KUPAMBANA NA MAHARAMIA WA TASNIA YA FILAMU NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye, jana akiwa kwenye moja ya maduka yanayouza kazi za sanaa (filamu) za nje bila kufuata sheria katika mtaa wa Kariakoo Jijini Dar es salaam.

Katika ukaguzi huo, Waziri Nnauye aliambatana na maofisa wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA, Bodi ya Bofilamu Tanzania, COSOTA, BASATA, Polisi pamoja na halmashauri lengo ikiwa ni kuhakikisha biashara haramu ya filamu za nje zinazouzwa nchini bila kukaguliwa na mamlaka husika na kuwa na stempu za TRA inatokomezwa kwani imekuwa ikiua soko la ndani na kuisababishia hasara serikali na hata wanatasnia wa ndani.

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na wadu mbalimbali ikiwemo Bodi ya Filamu nchini, Shirikisho la Filamu, TRA pamoja na polisi imedhamiria kuhakikisha uharamia wa kazi za sanaa hususani uuzwaji wa filamu za nje zisizokaguliwa na kupewa stempu za TRA unatokomezwa kwani umekuwa ukiisababishia hasara na kuua soko la tasnia hiyo nchini na hivyo kuwakosesha mapato pia wanatasnia hiyo wanchini.
#BMGHabari
Hii ni awamu ya pili ya ukaguzi wa kazi za sanaa zinazouzwa kinyemera nchini uliofanywa na Waziri Nnauye kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Bodi ya Filamu nchini ambapo mara zote shehena ya kazi bandia na zisizo na nembo za TRA zimekuwa zikikamatwa ambapo serikali imedhamiria kuziteketeza na kuwafikisha mahakamani wahusika wote.
Wakati huo huo juhudi za wadau wa sanaa nchini zinaendelea ili kuhakikisha sera ya filamu inakamilika ili kusaidia katika uendeshaji na usimamizi wa kazi za tasnia hiyo kwa ajili ya manufaa ya taifa na wanatasnia wote kwa ujumla.
Miongoni mwa duka lililokutwa likiuza filamu za nje kinyemera katika Mtaa wa Kariakoo Jijini Dar es salaam katika ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiambatana na maofisa mbalimbali ikiwemo kutoka Bodi ya Filamu nchini, TRA na polisi.

No comments:

Powered by Blogger.