LIVE STREAM ADS

Header Ads

MSIMAMO WA SERIKALI JUU YA MATUMIZI YA POMBE ZA VIROBA NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

James Salvatory, Dar
Serikali imesema siku ya kesho, Machi Mosi ni mwisho wa uuzaji wa pombe zinazofungwa kwenye vifungashio vya  plastiki (viroba), huku oparesheni ya kupiga marufuku uzalishaji, uingizaji, usambazaji na matumizi ya vifungashio vya plastiki (viroba) vya pombe kali hapa nchini ikipangwa kuanza Machi Mbili mwaka huu nchini kote.

Akizungumza leo na waandishi wa habari  Jijini dar es salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, amesema oparesheni hiyo itafanyika katika  mikoa yote ya Tanzania Bara.

Makamba ameongeza kuwa malighafi zote zinazoingizwa nchini lazima ziwe zimefuata taratibu za kisheria, kwa lengo la kuokoa mazingira na kudhibiti madhara ya kiafya kwa watumiaji.

Aidha ameowaomba wananchi kutoa taarifa za watu wanaozalishaji pombe kali zijulikanazo kama viroba, huku akiahidi zawadi nono kwa mwananchi yeyote atakayetoa taarifa hizo.

No comments:

Powered by Blogger.