LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA WAHIMIZWA KUSOMESHA WATOTO WA KIKE.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith  Ferdinand,Mwanza
Jamii mkoani Mwanza imeshauriwa kuwathamini na kuwapeleka shule watoto wa kike, ili kuweza kujikwamua kiuchumi  sambamba na kuwakinga na mimba za utotoni  ambazo hukatisha ndoto zao.

Ushauri huo ulitolewa jana na Mkurugenzi wa  Taasisi isiyo ya Kiserikali ya  Education for Better and Living (EBLI) Bernard Makachia, wakati akizungumza na wanahabari Jijini Mwanza kuhusu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na taasisi hiyo katika kuwasaidia watoto wa kike.

Makachia alisema ili kuweza kupunguza mimba za utotoni ni lazima  wazazi na walezi  kukemea vitendo vya  ukatili kwa watoto wa kike na kuhakikisha wanawapeleka shule ili kupata elimu ambayo ndiyo  urithi muhimu kwa maisha ya baadae.

 “Lengo la kuanzisha  kituo  hiki ni kuwasaidia  watoto waliokatishwa masomo   wakiwa bado wadogo kwani sisi tunawafundisha ujasiriamali, masomo ya tehama na biashara, ili  waweze kujiajiri wenyewe   na kuepuka kuwa tegemezi,” alisema Makachia.

Pia alisema, wananuia kutoa semina  kwa  jamii na wanafunzi,wakishirikiana na serikali,  ili kutokomeza  vitendo vya ukatili kwa  watoto wa  kike, kwa kufanya hivyo kutasaidia  kutimiza ndoto zao  ambazo  hukatishwa na wazazi kwa kuwathamini   wakiume  kulioko wao.

“Mimba za utotoni hazisababishwi na wanafunzi pekee yao bali hata kitendo cha wazazi kufumbia macho uovu huo na kuacha kuuripoti kwenye vyombo vya dola nako huchangia tatizo hili kukua, ni vyema tukaungana sote na kutokomeza vitendo hivyo,” alisema Makachia.

Taasisi ya Education for Better and living (EBLI) imejikita katika kuwasaidia watoto wa kike waliopata  mimba za utotoni kwa kuwapa elimu ya ujasiliamali, biashara na tehama ili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao za kupata elimu.

No comments:

Powered by Blogger.