LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAAMUZI YA MAHAKAMA YA RUFAA KATIKA HUKUMU YA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU JIMBO LA BUNDA MJINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Wakili wa wakata rufaa, Costantin Mtalemwa, akitoa ufafanuzi kwa wanahabari baada ya kesi ya rufaa ya kupinga matokeo jimbo la Bunda Mjini mkoani Mara kuahirishwa na Mahakama ya Rufaa hii leo Jijini Mwanza.

#BMGHabari
Mahakama ya Rufaa nchini imeanza kusikiliza maombi ya rufaa katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi Mkuu 2015 Jimbo la Bunda Mjini mkoani Mara iliyofunguliwa na wapiga kura wa jimbo hilo wakipinga ushindi wa mbunge Esther Bulaya.

Wakili wa waleta maombi, Costantin Mutalemwa, amesema hoja za rufaa hiyo ni za kisheria hivyo mahakama hiyo inaratarajia kupitia hoja zilizowasilishwa awali ili kujidhirisha ikiwa Mahakama Kuu ilitenda haki baada ya wateja wake kushindwa katika kesi hiyo.

"Majaji wa rufani wamesema itapangiwa kusikilizwa, lini hatujui, tutajulishwa. Waliposhtaki walisema hoja zao ni za kisheria na tuliwachapa kwa hiyo wameleta rufaa wamesema hoja zao ni za kisheria, tutawachapa vile vile. Amesema wakili wa mjibu maombi, Tundu Lisu.

Wapiga kura wanne wa jimbo la Bunda Mjini ambao ni Matwiga Matwiga, Magambo Masato, Janes Ezekiel na Acetic Malagila walifungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu jimbo la Bunda Mjini uliompa ushindi Esther Bulaya (Chadema) dhidi ya Steven Wasira (CCM) wakidai uchaguzi huo uligubikwa na kasoro kadhaa ikiwemo mgombea wa CCM kutotaarifiwa kwa maandishi wakati wa majumuisho ya kura ambapo rufaa hiyo.

Rufaa hiyo imeahirishwa hadi jumatatu ijayo ambapo Mahakama itatoa uamuzi wake wa kusikiliza maombi ya walalamikaji na ikiwa kama itasikilizwa Jijini Mwanza ama Jijini Dar es salaam kama walalamikaji walivyoomba.
Wakili wa mjibu maombi, Tundu Lisu, akiongea na wanahabari
Wakili wa mjibu maombi, Tundu Lisu, akitoka mahakamani
Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Bunda Mjini (CCM), Steven Wasira (kulia) akitoka mahakamani.
Taswira mahakamani

No comments:

Powered by Blogger.