LIVE STREAM ADS

Header Ads

MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI WATAKA RAIA WASITESWE.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

James Salvatory, Dar
Vyombo vya dola nchini vimeaswa kufuata misingi ya haki za binadamu na kuacha kuwatesa raia pindi vinapofanyapo upelelezi.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu  (THRDC), Onesmo Olengurumwa, ameyasema hayo kwenye warsha ya asasi za kiraia ya vkuanzisha mtandao  wa pamoja wa kupinga uteswaji na unyanyasaji kinyume cha haki za binadamu.

Amesema watuhumiwa wengi wamekua wakiteswa  na kunyimwa uhuru wa kijielezea kitendo ambacho kimekua kikipelekea kukosa haki zao za msingi kwa kulazimishwa kukubaliana na makosa ambayo siyo yao kutokana na hofu iliyoyojingeka katika jamii.

Aidha amesema kuwa asasi hiyo imeandaa jukumu la kuwafuatilia wale wote ambao waliteswa na kupata matatizo ya kisaikolojia pamoja na ulemavu uliotokana na kuteswa ili waweze kuwasaidia na kuondokana na hofu waliyonayo kwa sasa.

Naye wakili wa kujitegemea, Haroni Sungusia, amesema kuwa takwimu nyingi zimegubikwa na hofu kutokana na vitendo hivyo kufanywa na vyombo vya usalama ikiwemo jeshi la polisi
kitendo ambacho kimekuwa kifanywa kwa usiri mkubwa na kushindwa kupata takwimu sahihi.

No comments:

Powered by Blogger.