MKURUGENZI WA HABARI MAELEZO AFUNGA MAFUNZO YA TOVUTI KWA MAOFISA HABARI NA TEHAMA KANDA YA ZIWA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo/ Msemaji wa Serikali Dkt.Hassan Abbas, hii leo akizungumza wakati wa zoezi la kufunga mafunzo ya tovuti kwa maofisa habari na Tehama wa halmashauri na mikoa ya Kanda ya Ziwa yaliyoanza jumatatu iliyopita.
Kwenye uzinduzi wa tovuti za halmashauri na mikoa ya Kanda ya Ziwa, Dkt.Abbas amewasisitizia maofisa hao kuweka mipango, mikakati pamoja na utekelezaji wa miradi ya serikali na hata maoni ya wananchi kwenye tovuti hizo ili kuwarahisishia katika wananchi kupata taarifa muhimu kwa wakati.
Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Uimarishaji Mifumo wa Mawasiliano katika Sekta za Umma PS3, wenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa taarifa sahihi za serikali kupitia tovuti za halmashauri na mikoa nchini ambapo maofisa hao wamefunzwa kutengeneza na kusimamia tovuti hizo.
#BMGHabari
Washirikiwa mafunzo ya tovuti kwa maofisa habari na Tehama wa halmashauri na Mikoa ya Kanda ya Ziwa, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo/ Msemaji wa Serikali Dkt.Hassan Abbas, hii leo wakati akifunga mafunzo hayo yaliyoanza jumatatu iliyopita.
Mkuu wa Kitengo cha Mifumo wa Mawasiliano PS3 Dar es salaam, Desderi Wengaa, akitoa ufafanuzi kuhusiana na mafunzo ya tovuti kwa maafisa habari na maafisa Tehama wa halmashauri na mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo amesema lengo ni kuwajengea uwezo maofisa hao wa kuwafikishia wananchi taarifa muhimu za serikali kwa njia ta mtandao/ tovuti.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Tamisemi, Rebeca Kwandu, akizungumza kwenye ufungaji wa warsha hiyo ambapo amesema malalamiko ya wananchi kukosa taarifa muhimu za serikali ikiwemo za maendeleo yatapungua kutokana na taarifa hizo kuwekwa kwenye tovuti za halmashauri na mikoa kwa wakati. Amesisitiza tovuti hizo kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.
Afisa Habari halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Violancia Mbakile, akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo. Aliwashukuru wadau wote ikiwemo Tamisemi, PS3 na EGA kwa kuwafikishia mafunzo hayo na kuwasihi wanasemina wenzake kuyafanyia kazi kwa vitendo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo/ Msemaji wa Serikali Dkt.Hassan Abbas (wa tatu kushoto), akizindua tovuti za mifano zilizotengenezwa kwenye mafunzo hayo ikiwemo tovuti ya mkoa wa Mwanza.
Afisa Habari mkoani Mwanza, Atley Kuni, akiongoza zoezi la uzinduzi wa tovuti mbili za mfano ikiwemo ya mkoa wa Mwanza kwenye kilele cha mafunzo ya tovuti kwa maofisa habari na Tehama Kanda ya Ziwa.
No comments: