TAMTHILIA MPYA YA "INTERNATIONAL LOVE" KUZINDULIWA JIJINI MWANZA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Judith Ferdinand, Mwanza
Mkurugenzi wa kampuni ya African Cinema ambaye pia ni muigizaji wa filamu Tanzania Richard Kabisi, anatarajia kuzindua tamthilia inayo kwenda kwa jina la International Love.
Kabisi aliyabainisha hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya JB Belmont Jijini Mwanza.
Alisema tamthilia hiyo yenye ladha ya kiswahili na kihindi, imewashirikisha wasani kutoka Mwanza kwa asilimia kubwa akiwemo Khadija Saloon ambaye ni muhusika mkuu wa kike ambaye amecheza kwa jina la Careen huku yeye akitumia jina la John na ndiye muhusika mkuu wa kiume.
Alisema tamthilia hiyo itazinduliwa hivi karibuni mkoani hapa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye pamoja na wasanii wengine wanatarajiwa kuhudhuria.
Pia alisema itasaidia kuibuka vipaji na kuinua waigizaji wa Kanda ya Ziwa, kwani waigizaji wa tamthilia hiyo wanatoka Mwanza isipo kuwa yeye tu.
Hata hivyo alisema, bado wanafanya mazungumzo na kampuni ya Dstv kwa ajili ya kuanza kuonyeshwa tamthilia hiyo katika chaneli,ili watu wengi waweze kutazama,kuelimika, kuburudika, sambamba na kutambua vipaji vilivyopo Kanda ya Ziwa.
Hata hivyo alisema, ameamua kufanya tamthilia kutokana na kuwa na mashabiki wengi pamoja na kuendana na soko.
Naye Muongozaji wa tamthilia hiyo kutoka kampuni ya Mywood International Films, John Mlulu alisema, wameamua kufanya tamthilia ya international love iliyotumia lugha mbalimbali, ili kushawishi nchi nyingine kujifunza kiswahili.
Alisema tamthilia hiyo ni sehemu ya mraadi utakaozunguka sehemu mbalimbali kwani sehemu ya kwanza ya tamthilia hiyo itaishia Mwanza, na sehemu ya pili wanatarajia kufanyia Kenya na baadae katika mikoa mingine nchini, ili kuleta mabadiliko katika tasnia yatamthilia.
Kwa upande wake Khadija Saloon ambaye ni mmoja wa waigizaji wa tamthilia hiyo alisema, watanzaia waangalie tamthilia hiyo ni yakimataifa haijawai kutokea nchini, pia matendo katika uigizaji yanaendana na uhalisia.
Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fissoo, akizungumza hivi karibuni Jijini Mwanza, kwenye mafunzo kwa wanatasnia wa filamu mkoani Mwanza ili kuwawezesha kuzalisha kazi zenye ubora.

No comments: