LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA MUHIMU KUTOKA WIZARA YA AFYA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

James Salvatory, Dar
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imevifuta vituo vyote vinavyotoa huduma za afya ya VVU na Ukimwi kwa makundi maalumu  baada ya kubainika kwamba vituo hivyo vinahusika na kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja na ushoga.

Akizungumza jana na wandishi wa habari Jijini Dar es salaam waziri wa wizara hiyo. Ummy Mwalimu alisema serikali haitavitambua vituo hivyo kwani baadhi yake vimekuwa vikihamasisha mapenzi ya jinsia moja na badala yake huduma hizo  zitasimamiwa na mwongozo mpya wa mwaka 2017 na huduma za kupambana na virus vya ukimwi katika makundi ya madawa ya kulevya na watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja vitaendelea kutolewa na vituo vya afya hususani zahanati na hospitali.

No comments:

Powered by Blogger.