LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAFUNDI WENYE ULEMAVU MKOANI MWANZA WAILILIA SERIKALI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Mafundi wenye ulemavu mkoani Mwanza wameiomba serikali kuwapa mikopo ili waweze  kujiendesha katika shughuli zao  za kiuchumi na  kuacha kuwa ombanba sambamba na tegemezi kwenye familia.

Hayo yalisenwa jana na  mafundi wa Karakana ya Nyakato Tri-cyle Work Shop iliyopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza wakati wakizungumza na BMG.

Mmoja wa mafundi hao John Kerenge alisema, serikali ikiwawezesha Walemavu kwa kuwapa  mikopo, ili waweze kujiingizia  kipato  kupitia ujuzi walionao itasaidia kupunguza ombaomba na tegemezi kuanzia ngazi ya familia.

“Nasikitika kuona watu wanakaa barabarani  kwa lengo la  kuomba, kufanya hivyo siyo vizuri  kwani  kuna kazi nyingi ambazo watu wenye ulemavu   wanaweza kufanya na kujipatia kipato,haipendezi kuwategemezi kwa watu,”alisema Kerenge.

Pia aliiomba serikali, kuwapatia tenda pindi itakapo kuwa na kazi za kutengeneza madawati, madirisha, meza  za kuchomelea,  ili  wajipatie kipato kwani wakiwezeshwa wanaweza. 

Kwa upande wa  fundi wa kalakana hiyo   Veronica Mtiro alisema, serikali imewasahau  katika kuwapa mikopo kwani  mtaji walionao ni mdogo, hali  inayosababisha    kushindwa  kukamilisha  kazi kwa wakati  pale wanapopata tena.

“Tunaiomba serikali  itukumbuke na sisi, kwa kutupa mikopo kwani tuna mtaji kidogo ambao unashindwa kukidhi matakwa,pindi tunapota wateja wengi kwa wakati mmoja,"alisema Mtiro.

Hata hivyo Mabulla Erest alisema , kalakana hiyo  inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo masoko na mtaji  kwani  kuchangia  kukwamisha maendeleo ya shughuli zao.

No comments:

Powered by Blogger.