TAASISI YA METDO TANZANIA YA JIJINI MWANZA YAWASHAURI WAKULIMA KUBADILI MFUNO WAO WA KILIMO.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Mkurugenzi wa Taasisi ya Metdo Tanzania, Ashraf Omary (kulia), akizungumza na mwanahabari wa Lake Fm Mwanza, George Binagi-GB Pazzo.
#LakeFmHabari
Wakulima
mkoani Mwanza wameshauriwa kubadili mfumo wa kilimo kwa kuachana na kilimo cha
kutegemea mvua na badala yake wajikite kwenye kilimo cha umwagiliaji ambacho
kina tija zaidi.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Metdo Tanzania ya Jijini Mwanza inayoshughulisha na utoaji wa
elimu ya mazingira katika maeneo ya migodini, Ashraf Omar, alitoa ushauri huo jana wakati akizungumza na Lake Fm.
Alisema
kwa idhini ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, taasisi hiyo imepewa
ridhaa ya kufanya tafiti za kilimo na kutoa elimu katika jamii juu ya kilimo cha
umwagiliaji hivyo wakulima wanapaswa kuitumia ipasavyo ili kuboresha shughuli
zao.
Tayari
taasisi ya Metdo Tanzania imeanza kufanya tafiti za kilimo cha umwagiliaji
katika halmashauri ya wilaya ya misungwi katika eneo la Mbalika ambako
mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Eliud Mwaiteleke, anahimiza kilimo cha
umwagiliaji kufanyika kwa manufaa ya jamii hususani akina mama na vijana.
No comments: