LIVE STREAM ADS

Header Ads

KUELEKEA KILELE CHA MAONYESHO YA VIWANDA VIDOGO NA KATI KANDA YA ZIWA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Dkt. Leonard Masale, kuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa maonyesho ya 14 ya Viwanda vidogo na vya Kati Kanda ya Ziwa.

Maonyesho hayo yameandaliwa na Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo Tanzania ( SIDO) ofisi za mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa kushirikiana na ofisi ya mkoa Mwanza, yanayofanyika katika uwanja wa Furahisha uliopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza, yatafikia tamati Machi  30 mwaka huu.

Akizungumza na BMG Kaimu Meneja wa SIDO mkoa wa Mwanza Emmanuel Ngoyinde amesema, maonyesho hayo yanafanyika kwa siku 6, ambayo yalianza machi 25 na kufikia tamati machi 30, na mgeni rasmi atakua Mkuu wa wilaya ya Ilemela Dkt. Masale

Ngoyinde amesema, maonyesho hayo ni ya sita kimkoa na 14 kikanda, ambayo yamewakutanisha wajasiriamali  176 kutoka Kanda ya Ziwa na mikoa jirani ikiwemo Dar es salaam, taasisi za serikali 13 na makampuni binafsi matano.

Pia amesema, lengo la maonyesho ni kuwakutanisha wajasiriamali na wateja moja kwa moja,pamoja na kubadilishana ujuzi na kuelimisha wao wenyewe.

Hata hivyo amesema, muitikio wa wananchi ni mkubwa, amewaomba wasiishie kuangalia bidhaa  ila wanunue ili kuwaunga mkono na kuinua uchumi wa taifa.

No comments:

Powered by Blogger.