LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAASISI YA GS1 YAFUNGUA MILANGO KWA WAJASIRIAMALI NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Wajasiriamali nchini wamehimizwa kujiunga na taasisi  ya  GS1, kwa ajili ya kutumia Misimbomilia( Barcode) katika bidhaa wanazozalisha, ili kupanua wigo wa biashara.

Wito huo umetolewa na Afisa Masoko wa GS1 Tanzania Mussa Funding wakati akizungumza na BMG kwenye maonyesho ya 14 ya viwanda vidogo na kati Kanda ya Ziwa yanayofanyika katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.

Fundi amesema, GS1 ni taasisi iliyopewa mamlaka na serikali ya kutoa  Barcode, inayosaidia kupanua wigo wa biashara kwa kuuza bidhaa sehemu mbalimbali, ikiwemo  supermarket na nje ya nchi.

Pia amesema,Barcode itamsaidia mjasiriamali kujua bidhaa zake zinavyokubalika na wauzaji wa rejareja ulimwenguni, rahisi kujua mtiririko wa bidhaa zinazoingia na kutoka,kuongeza ukubwa wa soko na nafasi ya kufanya biashara.

Hata hivyo amesema, mjasirimali au mfanyabiashara anatakiwa awe na leseni ya biashara, TIN namba pamoja na usajili wa biashara au kampuni, ili aweze kupatiwa Barcode ambayo inakiambishi awani 620.

"Mpaka sasa taasisi yetu imesajili wanachama zaidi ya 1000, wanaotumia Barcode kiambishi awani 620," amesema Fundi.

Aidha amesema, wameanzisha mradi kwa ajili ya kuwaelimisha wajasiriamali katika halmashauri zote nchini kuhusu umuhimu na namna ya kutumia Barcode.

No comments:

Powered by Blogger.