LIVE STREAM ADS

Header Ads

UONGOZI WA UWANJA WA CCM KIRUMBA WAKANUSHA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Uongozi wa Uwanja wa CCM Kirumba,umeshangazwa na taarifa zilizoenea juu ya zuio la CAF kwa mechi ya Yanga FC  na Mc Alger kwenye uwanja huo.

Hayo yamesemwa na Meneja wa uwanja wa CCM Kirumba Steven Shija wakati akizungumza na BMG, ofisini kwake wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

"Kwanza, taarifa za awali za mchezo  huo,hatukuzipata rasmi zaidi ya kuziona kwenye mitandao  ya kijamii kama wengine walivyoziona,  na tarehe  8/04/2017  ambayo imetajwa kama ndio siku ya mchezo huo,ilikuwa ni tarehe ya kuchezwa mechi  kati ya Mbao FC na Simba FC ambayo imesogezwa mbele mpaka aprili 10,mwaka huu,kwa taarifa tulizonazo ni kutokana na tarehe ya awali kuingiliana na shughuri nyingine za kijamii ndani ya uwanja," amesema Shija.

Shija amesema, tangu taarifa  imetoka juu ya Mechi hiyo, uongozi wa uwanja umekua ukipokea ugeni kutoka CAF kwa ukaguzi wa uwanja,ambapo mpaka sasa Mkaguzi  Maxwell Mtouga  amekuwa akifika mara kwa mara uwanjani kukagua maendeleo ya Ukarabati ambao unapaswa kukamilika aprili 10 mwaka 2017 kwenye maeneo muhimu aliyoyaainisha.

Hivyo amesema,uongozi wa uwanja huo, haukua na  taarifa rasmi zilizokuwa zimefika juu ya mechi hiyo ya Kimataifa kuchezwa katika uwanja huo, kama taarifa zilivyokuwa.

Aidha amesema,uongozi wa uwanja huo,  wamewahakikishia wadau wa michezo ndani na nje ya  mkoa wa Mwanza  kuwa maelekezo yote yaliyotolewa na Mkaguzi wa CAF  Mtouga yameanza kufanyiwa kazi.

No comments:

Powered by Blogger.