UTPC YANG'AKA SAKATA LA MAKONDA KUVAMIA CLOUDS TV AKIWA NA BUNDUKI.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Judith Ferdinand, Mwanza
Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini (UTPC), umelaani kitendo kilichofanywa na kuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda cha kuingia studio za runinga cha Clouds wikendi iliyopita.
Hayo yamesemwa leo na Rais wa UTPC, Deogratias Nsokolo (kushoto), wakati akizungumza na wanahabari katika ofisi ya umoja huo Jijini Mwanza.
"Kitendo cha kiongozi wa serikali kuvamia chombo cha habari akiambatana na askari wenye silaha, ni jambo baya sana,hivyo sisi waandishi wa habari na wadau wetu, lazima tukilaani kwa nguvu zetu,kwani tukio kama hili halijawai kutokea nchini, " alisema Nsokolo.
Nsokolo amesema, mtu yoyote anayetaka kulazimisha habari gani itoke au isitoke,anakua anafinya uhuru wa habari, kwani kazi ya uandishi ina miiko ambayo ndio inatumika kuchagua habari ya ipi itumike ipi isitumike.
Pia amesema, ni wajibu wa waandishi wa habari na wadau wanaopenda maendeleo, kuulinda uhuru wa habari kwa faida ya nchi, sambamba na kutoa pole kwa wamiliki na wafanyakazi wa clouds kwa kuwatia moyo wa kuendelea na kazi ya kujenga taifa.
Hata hivyo ametoa wito kwa wadau,viongozi wa kisiasa na kiserikali kuviheshimu vyombo vya habari na wavisaidie ili vitimize wajibu wao bila vikwazo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan (kulia), amesema mwandishi kuandika habari akiwa amesimamiwa na magwanda ya kijeshi siyo vionjo vya habari, pia nchi imevunja rekodi ya mkuu wa mkoa kuingia studio za chombo cha habari.

No comments: