LIVE STREAM ADS

Header Ads

WITO WA NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

James Salvatory, Dar
Wito umetolewa kwa Wananchi na Jamii kwa ujumla kuachana na Sanaa ambazo zina akisi mila na Desturi nakusababisha kumdhalilisha mwanamke ambazo ni taarabu,ngoma,muziki,michezo ya kuigiza na filamu.

Akizungumza leo na wanahabri jijini Dar es salaam Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura amesema kuwa Ngoma kama vile Kigodoro,Khangamoko,Khanga Ndembendembe,na nyinginezio ambazo huchezwa hadharan zinakiuka kwa kiasi kikubwa maadili,mila na Desti za Mtanzania.

Aidha amesema kuwa jamii inakumbushwa kufuata Sheria,Kanuni na taratibu bila shuruti,nakwamba ukiuukaji wa sheria ni kosa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakekiuka.

Aidha amesema kuwa Serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) itaendlea kubaini,kuenzi,kukuza,kuhidfadhi na kurithisha Utamaduni na Sanaa zenye kuzingatia na kuimarisha Maadili,Mila na Desturi, kwa kuleta maendeleo,kwa wanachi ambao wanajihusisha na fani mbalimbali za Sanaa na Utamaduni ikiwemo ngoma za asili,filamu,muziki,Jando,Unyago,Matambiko,Sherehe na Maadhimisho mbalimbali.

No comments:

Powered by Blogger.