LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKURUGENZI BOA BANK ATOA RAI KWA WATANZANIA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

 Na James Salvatory, BMG
Watanzania wametakiwa kuzitumia vyema fursa za kifedha hapa nchini ili kujikwamua kiuchumi.

Hayo yalisemwa jana na Kaimu Mkurugenzi wa benki ya Africa (BOA BANK) Wasia Mushi, wakati akizungumza na wanahabari katika hafla fupi ya benki hiyo ya kutimiza miaka 13 tangu kuanzishwa kwake  hapa nchini mwaka 2007.

Alisema kama wananchi watazitumia fursa za kifedha ikiwemo kupata mikopo na kuitumia katika malengo walioyakusudia mikopo hiyo itawasaidia wananchi hao kufanikiwa hasa katika biashara na hatimaye kurejesha mikopo yao bila kupata hasara katika biashara zao.

Benki hiyo imekuza mtaji wake kutoka bilion 3 mwaka 2007 mpaka kufikia bilioni 37 mwaka 2017 na imewekeza katika nchi 18 ikiwemo nchi ukanda wa afrika ya kati,ukanda wa afrika mashariki na bahari ya hindi ikiwemo Tanzania ambapo kwa Tanzanja benki hiyo ina matawi 27 huku matawi 14 yakiwa jijjni Dar es salaam na 13 mikoani na ina wateja wapatao laki moja na arobaini huku amana yake ikiwa ni bilioni 325No comments:

Powered by Blogger.