LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWILI WA PROFESA BINAGI WAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM KUELEKEA MKOANI MARA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Katikati ni mke wa marehemu Profesa Binagi, akiwa na wanafamilia wengine wakiuaga mwili wa marehemu hii leo Jijini Dar es salaam ili kusafirishwa kwenda mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.
Picha na Msubi Binagi

#BMGHabari
Ndugu, jamaa na marafiki hii leo jumatano April 05,2017 wameuaga mwili wa marehemu Profesa Lloyd Manamba Binagi aliyefariki ghafla juzi jumatatu April 03,2017 Jijini Dar es salaam, kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.

Mwili huo utapokelewa kesho asubuhi katika uwanja wa ndege Jijini Mwanza, na baadaye kusafirishwa kwenda nyumbani kwa marehemu Bomani wilayani Tarime.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika katika malalo ya Binagi yaliyopo Kenyamanyori wilayani Tarime siku ya jumapili, April 09,2017 baada ya familia ya marehemu kuwa imewasili kutoka nchini Marekani.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina!

No comments:

Powered by Blogger.