LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYANI ILEMELA KUFANYA UCHAGUZI MWEZI HUU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Chama cha Mapinduzi (CCM),wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, kinatarajia kufanya uchaguzi ngazi ya shina kati ya  April I7 hadi  30 mwaka huu.

Uchaguzi huo ambao utashirikisha mashina 3875 yaliyopo ndani ya wilaya hiyo, kwa kuchagua Mwenyekiti Shina ambaye ndiye  balozi pamoja na wajumbe  wanne wa kamati ya shina.

Hayo yamebainishwa leo na Katibu Wa CCM wilaya ya Ilemela Acheni Maulid  wakati akizungumza na BMG ofisini kwake wilayani humo mkoani hapa.

Maulid amesema, zoezi la kuchukua na kurudisha fomu kwa wagombea limekamilika jana Aprili 5,ambapo watu 5487 wamejitokeza  kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti huku 12789 nafasi ya wajumbe.

Pia amesema, hali ya uchukuaji fomu ni  nzuri, hivyo kupitia halmashauri kuu ya tawi husika Aprili 10 hadi 13, watakua na kikao cha kuchuja wagombea na Aprili 14 hadi 16 itatumika kwa wagombea kufanya kampeni na kujinadi kwa wanachama ambao ndio wapiga kura.

Hata hivyo amesema, mtu atakayepewa nafasi ya kugombea, anatakiwa kuwa mwanachama hai,mwenye uzoefu ndani ya chama pamoja na kutotumia rushwa.

Aidha amesema,wamejipanga kuhakikisha  uchaguzi unakuwa wa haki,kwa kusimamia idadi ya wanachama ndio watakao piga kura.

Vilevile amesema,amewataka Makatibu Kata  kuhamasisha wagombea kuepuka kutumia rushwa,kwani wamegundua ndio chanzo cha kuchagua viongozi wabovu.

"Kwa mgombea yoyote atakayebainika ametumia rushwa wakati wa kugombea am a kuchaguliwa,watafuta uteuzi wake,kama maelekezo ya Mwenyekiti  wetu taifa John Magufuli yanavyotutaka kufanya," amesema Maulid.

No comments:

Powered by Blogger.