LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHUKURANI KWA MWENYEKITI WA CCM TAIFA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wilaya ya Ilemela Acheni Maulid, amemshukuru Mwenyekiti wa chama hicho taifa John Magufuli,kwa kumteua pamoja na kumuacha wilayani humo.

Maulidi amesema hayo leo,wakati akizungumza na BMG ofisini  kwake wilayani Ilemela mkoani hapa.

" Napenda kutoa shukrani zangu kwa, Mwenyezi Mungu, Mwenyekiti wetu  taifa Magufuli,Katibu Mkuu pamoja na kamati kuu,kwa kuniteua tena kuwa Katibu  na kuniacha wilayani Ilemela," amesema Maulid.

Pia amesema, atafanya kazi kwa kushirikiana na viongozi wenzake, kuhakikisha uchaguzi wa chama hicho,  kuanzia ngazi ya shina mpaka wilaya unafanikiwa.

Hata hivyo amewashukuru wanachama na wanailemela kwa kumpa ushirikiano,hivyo kuhakikisha wanafanya vizuri katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na kupata viongozi bora na siyo bora kiongozi.

No comments:

Powered by Blogger.