TRL YAANZISHA SAFARI ZA TREN YA MIZINGO DAR - DODOMA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Na James Salvatory
Shirika la reli Tanzania (TRL) jana limeanzisha safari za treni ya mizingo (FLAG OFF) ya shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) lenye lengo la kuhudumia wateja kwa kiasi na muda unaoridhisha na kufikisha bidhaa kwa walaji wake.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa TRA, Masanja Kadogos,a alisema kihistoria huduma hiyo ilikuwepo tangu enzi za shirika la reli Tanzania TRC na katika mwaka 2004 ilikuwa imeshasafirisha jumla ya tani 400,723 za WFP na kuanzia mwaka 2006 ukashuka kutoka tani 66,994 hadi tani 846 kwa mwaka 2015.
Aidha alisema kuwa moja kati ya changamoto iliyopo ni ukosefu wa vichwa vya Tren vya kutosha na mabehewa Hata hivyo baada ya kujipanga na kuihakikishia huduma zinakamirika kusafirishia tani 7000 za mahindi kupeleka katika ghala kuu la WFP iliyoko Kiota Dodoma .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya TRL, John Kondoro, alisema kuwa tangu mwaka 2000 hii ni mara ya pili shirika hilo linasafirisha mizigo na kwa sasa wamesafirisha mzigo mkubwa na hii ikiwa ni faida maana inaongeza faida kwa shirika na kwa kufika hatua hiyo imani kubwa inajengeka kwa wadau kwa kazi hii inayofanyaka.



No comments: