USIYOYAJUA KUMHUSU MTANGAZAJI WA STORM FM YA GEITA, JOEL MADUKA.
"Tarehe 4 ya mwezi Aprili ni siku ambayo Mama Yangu Kipenzi alinileta Duniani Kiukweli ninakoswa maneneo ya kuandika lakini inabidi niandike juu ya siku hii ambayo kwangu ni muhimu.
Kwanza Nianze kwa kumshukuru MUNGU wangu ambaye ni Muumba wa Mbingu na Duniani kwa kunilinda tangu nazaliwa hadi siku hii ya leo hakika amekuwa mwaminifu kwangu amenifanyia amani na furaha.
Na pia Nakushuruku sana Mama yangu Kipenzi Eva Joseph Lyaka ,hakika mama umefanyika kuwa baraka kwangu kwani wewe ni mtu ambaye kwanza ulinifundisha upendo kwa watu wote na kumheshimu kila mtu haijalishi uwezo wake.
Nakumbuka umenisomesha kwa shida sana uliuza vitumbua,maandazi na muda mwingine kujitwika mahindi kupeleka mjini kuuza ili mradi tu uhakikishe mwanao nakuwa na msingi wa maisha siku zote ukukubari kushindwa ulikuwa ni mtu mwenye Bidii na maalifa na ambaye ulipenda kuona kile unachokifanya kinafanikiwa haijalishi wakati au eneo gani gumu ambalo ulipitia lakini ulisimama kama Mama Jasiri usiyekata tamaa kwa kuakikisha watoto wako wanafanikiwa.
Hahakika umekuwa ni mfano wa kuigwa Kwangu pamoja na Ndugu zangu,Seleman,Samsoni,Sospeter Lyaka,Devid na Dominica.Siku zote tunakuakikishia kukupenda daima na milele.
Nitakuwa mchoyo wa Fadhira nisipo mtaja Bibi yangu kipenzi mshauri wangu Anna Daud Lyaka hakika wewe ni Bibi wa kipekee jambo kubwa ambalo linaniongoza ambalo ulinifundisha ni kumtumainia Mungu siku zote za maisha yangu ya Dunia hata kama kuna mlima gani ulinifundisha nisimwache Mungu.
Bibi najua umri wako umekwenda lakini mawazo yako na hekima ya kipekee Mungu alivyokupatia ni Nguzo kubwa maishani Kwangu na pia ni taa na mwangaza siku zote za uhai wangu Bibi ni mengi ninayo ya kuandika juu yako lakini kwa leo naomba kuishia hapa.
Mke wangu ,Mwandani wangu,Msiri wangu,My Lazizi wangu, #FirstLadywangu Mama wa mwanangu Isaac ninamajina mengi sana Mke wangu Debora J Mkama ya kukuita lakini Kubwa zaidi Nakupenda na nitakupenda hadi mwisho wa maisha yangu.
Naweza nikasema wewe umekuwa ni baraka kubwa sana kwenye maisha yangu ulinikuta naitwa Joel lakini kwasasa Naitwa Baba Isaac ulinikuta ni bachera lakini kwasasa naitwa Mume wa Debora Katika siku yangu hii muhimu napenda kuchukua fursa hii kukushuru sana kwani umekuwa ni zaidi ya mwandani wangu naweza nikasema wewe umekuwa ni zaidi hata ya rafiki yangu kwangu ulinikuta sina kitambi nikiwa mwembamba lakini tangu nilipokuoa hata mwili wangu umebadirika na ndio maana muda mwingine nakwambia Punguza kupika vyakula vya kunenepesha nahitaji nirudi kama zamani ingawa inashindikana.
Mke wangu kubwa zaidi nakupenda na nakuombea kwa Mungu hakupe maisha marefu na yenye baraka tele na uwendelee kuwa mama bora wa familia.
Siwezi kumsahau Mwangu na kijana wangu wa kipekee ambaye ninampenda sana Isaac Joel ni mtoto ambaye Mungu ametupatia katika familia yetu kiukweli amekuwa baraka sana ndani ya familia yetu ni mtoto ambaye tunafurahia sana kuwa naye kwani amekuwa baraka kubwa kwenye familia yetu Nakuombea sana Mwangu Mungu akulinde na hukue ukimtegemea yeye siku zote za uhai wako kwani hayupo ambaye amemtumaini yeye hakumuacha kamwe.
Asante kwa Wafanyakazi pamoja na wakuu wangu wa kazi wa kituo chetu pendwa cha 88.9 storm fm nyie ni miongoni mwa familia yangu naamini mmefanyika baraka sana kwangu tuendelee kuwa bega kwa bega kuakikisha malengo yetu tuliyonayo kwenye kampuni yanatimia siku zote palipo na umoja kunaushindi.
Shurani zingine ziwaendee familia hizi mbili ya Mr &Mrs George Binagi GB Pazzo na Mr&Mrs Sospeter Lyaka nyie ni watu muhimu sana kwangu.
Asanteni sana wadau wangu wa nguvu wa mtandao wenu pendwa wa Maduka online.blogspot.com niseme tupo pamoja .
Asanteni sana marafiki zangu mimi pamoja na familia yangu tunawapenda sana na tupo pamoja kwa kila hatua.
Ninayo mengi ya kuandika naamini nikiandika nitajaza kurasa lakini mwisho wa siku kitakuwa ni kitabu sio post tena kwa leo naomba niishie hapo". Joel Maduka.
No comments: