LIVE STREAM ADS

Header Ads

Uwanja wa CCM Kirumba kuwa na hadhi ya kimataifa.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Judith Ferdinand, Mwanza
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mwanza Raymond Mwangwala,amehaidi kuufanya uwanja wa CCM Kirumba kuwa na hadhi ya kimataifa.

Mwangwala aliyasema hayo jana, wakati akipokea maelezo ya namna mradi wa ukarabati wa uwanja huo unavyoendelea kutoka kwa Meneja wa uwanja wa CCM Kirumba Steven Shija mara baada ya kufanya ziara uwanjani hapo.

Alisema,uwanja wa CCM Kirumba unasifika nchini,hivyo kutokana na dosari zilizojitokeza, hata hakikisha anazitatua na uwanja huo kuwa na hadhi ya kimataifa akishirikiana na uongozi wa uwanja huo.

" Ukitoka sehemu ambayo ulikuta uwanja ni wakaida,halafu ukauwacha ukiwa na hadhi ya kimataifa, hiyo ni heshima kubwa,hivyo nitaakikisha changamoto zilizopo zinatatuliwa na kufikia lengo," alisema Mwangwala.

Pia alisema, kwa kuwa kuna mikakati ambayo wataifanyia kazi na kuhakikisha Mwanza inakua ndio kituo cha michezo ya kimataifa.

Hata hivyo aliasema,ataangalia changamoto ya kisima kilichopo ndani ya uwanja huo,ili wajue namna ya kutatua,jambo litakalosaidia upatikanaji wa maji.

Kwa upande wake Shija alisema, Chama cha Soka Barani  Afrika (CAF), walifanya ukaguzi katika uwanja huo na kubaini mapungufu ambayo baadhi yameanza kufanyiwa kazi,ili kuweza kukidhi hadhi ya kimataifa,ambapo walitakiwa kufikia tarehe 10 Aprili mwaka huu, yaweyamekamilika lakini wameomba kuongezewa muda.

Aidha alisema, mpaka sasa wameanza ukarabati wa choo  kimoja kimoja kulingana na uhitaji wa watu  wa kuendelea kutumia kukidhi haja zao,hivyo hawawezi kubomoa vyote kwa wakati  mmoja.

No comments:

Powered by Blogger.