LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA NCHINI WAPEWA SIRI KUKUZA BEI YA ZAO HILO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand,Mwanza
Wakulima  na  Wadau wa  zao la Pamba nchini,wametakiwa kuboresha zao hilo,ili kuuza kwa bei nzuri.

Hayo yalisemwa juzi na  Mkurugenzi Mkuu wa  Bodi ya  Pamba Tanzania, Michael Mtunga mwenye kikao cha wadau wa zao hilo,kilichofanyika Nyakahoja jijini Mwanza, chenye lengo la kuwajuza kuhusu shughuli za utafiti zinazofanywa na Balaza la Kilimo Tanzania (ACT), hasa katika kuchunguza athari za udhibiti wa zao hilo kwenye mnyororo mzima wa  thamani.

Mtunga alisema, mfumo wa baraza la  kilimo,unalengo la kuboresha zao hilo,ili liwe na ubora unaotakiwa, sambamba na kuiomba serikali  kuendelea kufanya juhudi za kuhakikisha zao hilo linakua.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) Janet Bitegeko alisema, wamefanya utafiti ambao umebaini uwepo wa tozo kubwa kutoka TRA,halmashauri kuwa na tozo nyingi pamoja na wadhibiti wa zao hilo, ambazo ndio zinachangia pamba kushuka,hivyo kuna haja ya serikali kuangalia na kufanyia kazi changamoto hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Usimamizi Bodi ya Pamba Tanzania James Shimbe alisema, Bodi imejidhatiti kuwa na mfumo utakaosaidia hupatikanaji wa pembejeo pamoja na viuatilifu,ili kuboresha zao hilo na kuweza kupata pamba nyingi itakayotumika katika viwanda nchini na kuuza nguo nje ya nchi.

Pia amesema, ili kuboresha zao hilo Bodi inatoa mafunzo kwa wakaguzi Wa zao hilo ngazi ya wilaya,ili wakawafundishe wakulima wawezeshaji vijijini namna ya kutumi pembejeo na viuatilifu ambao nao watawaelimisha wakulima wengine,jambo litakalosaidia kutatua tatizo lililopo.

Aidha Katibu  Mkuu wa Chama cha Wakulima wa Pamba TanzaniaGeorge Mpandujia aliiomba, serikali kuongeza maafisa  ugani ,ambao wataweza kuwafikia wakulima na kuwashauri namna ya kuendeleza na kuboresha zao hilo.

Vilevile  Mshauri  Mwelekezi wa zao hiloPrf.Reuben Kadigi alisema, lengo la kukutana na wadau ni kupata matokeo mazuri ya pamba,sambamba na kuiomba serikali kuboresha vyombo vya udhibiti wa zao hilo.

Hata hivyo mmoja wa wakulima wa zao hilo kutoka  Maswa Lupande Nillah alisema, ili kilimo cha Pamba kilete tija serikali inatakiwa kupunguza tozo,pamoja na kuwaelimisha wakulima namna kilimo bora ambacho kitasaidia kupataa mazao na kumudu maisha.

No comments:

Powered by Blogger.