DIWANI WA KATA YA BUZURUGA JIJINI MWANZA AONGOZA WAKAZI WA KATA HIYO KUADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI KATIKA KITUO CHA AFYA BUZURUGA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mwananzengo wakiongea na Lake Fm kuhusiana na usafi huo
Diwani wa Kata ya Buzuruga Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Richard Machema (kushoto), akishiriki zoezi la usafi pamoja na Wananzengo wengine wa Kata hiyo katika Kituo cha Afya Buzuruga hii leo, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, 2017.
BMGHabari
Wananzengo wa Kata ya Buzuruga wakiwa pamoja na diwani wao, Richard Machema (mwenye kofia), katika zoezi la usafi kwenye Kituo cha Afya Buzuruga hii leo, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, 2017.
Zoezi la usafi la kuondoa vichaka na taka katika mazingira ya Kituo cha Afya Buzuruga limeelezwa kusaidia kuteketeza maficho ya masalia ya mbu pamoja na baadhi ya vijana wasio na maadili mema waliokuwa na desturi ya kujificha kwenye vichaka hivyo kwa sababu mbalimbali ikiwemo uvutaji wa bangi.
Uteketezaji wa taka hatarishi ikiwemo chupa umelalamikiwa na wakazi wa Kata ya Buzuruga na kuomba suala hilo kufanyiwa kazi ili kuwa na uteketezaji taka usio hatarishi katika jamii
Usafi ukiendelea
Usafi ukiendelea
Mwananzengo wakiongea na Lake Fm kuhusiana na usafi huo
George Binagi-GB Pazzo
Diwani wa Kata ya Buzuruga Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Richard Machemba, amewakutanisha pamoja wakazi wa Kata hiyo na kufanya usafi wa mazingira katika Kituo cha Afya Buzuruga ili kuondoa hatari ya vichaka kituoni hapo.
Diwani wa Kata ya Buzuruga Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Richard Machemba, amewakutanisha pamoja wakazi wa Kata hiyo na kufanya usafi wa mazingira katika Kituo cha Afya Buzuruga ili kuondoa hatari ya vichaka kituoni hapo.
Akizungumza
wakati wa zoezi hilo, Machemba amesema uamuzi huo umefanyika ikiwa ni sehemu ya
kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani hii leo na kwamba hatua
hiyo pia itasaidia kuondoa hatari za kimazingira ikiwemo magonjwa kituoni hapo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Afya Kituo cha Afya Buzuruga, Daniel Buluya, amesema awali
mazingira ya Kituo hicho hayakuwa salama hatua ambayo ilikuwa inahatarisha
usalama wa wagonjwa na watumishi wa afya kituoni hapo.
Maadhimisho
ya Siku ya Wafanyakazi Duniani huadhimishwa kila mwaka Mei Mosi ili kutoa
mwanya wkwa wafanyakazi pamoja na viongozi mbalimbali kutafakari changamaoto zinazowakabiri
wafanyakazi na namna ya kuzitafutia ufumbuzi ambapo Kitaifa maadhimisho hayo
yamefanyika Moshi mkoani Kilimanjaro huku kauli mbiu ikiwa ni "Katiba na Utawala, Vizingatie Haki na Maslahi ya Wafanyakazi".
Tazama Video hapo chini
No comments: