LIVE STREAM ADS

Header Ads

IFAHAMU APPLICATION MPYA IITWAYO SIKILIZA NA MANUFAA YAKE.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Jalilu Zaid
Habari ndugu msomaji wa tovuti yako pendwa, kuna habari nzuri ambayo nahitaji kukushirikisha leo hapa hapa.

Habari yenyewe inaihusu Application ambayo sasa hivi umerahisishiwa zaidi na unaweza kusikiliza Kipindi chochote cha redio unachokipenda kutoka katika redio yoyote ambayo unaipenda hapa Tanzania na nje pia.

Kupitia App hii utaweza kuziskiliza redio zote ukiwa ndani ama nje ya Tanzania na kwa urahisi zaidi bila kusumbuliwa na kitu chochote.

Baadhi ya sifa za Application hii ambayo unaweza kusikiliza Redio.
1.  Orodha ya Redio zote unazohitaji kuziskiliza.
Kupitia Application ya SIKILIZA redio zote zimewekwa katika Orodha ambayo inakupa wewe urahisi wa kuchagua Redio ambayo utasikiliza kwa uharaka zaidi.

2. Redio zimetengwa kutokana na Mkoa ilipo.
Kitu kizuri kuhusu hii Application ya SIKILIZA Redio zote zinazopatikana kupitia Application hii zimetengwa kimkoa, Kwenye App ya SIKILIZA ipo sehemu ambayo inaonesha kabisa Mkoa ambapo Redio fulani inapatikana na hii inakurahisishia wewe kama unahitaji kusikiliza Redio yoyote kutoka mkoa wowote unaouhitaji wewe.

3.  Ni rahisi kuitumia App hii ya SIKILIZA.
Application hii yenye Redio zote za Tanzania ni rahisi sana kutumia kwa sababu haina mkanganyiko katika utumizi wake.

4.Katika matumizi yake haitumii DATA nyingi. Ni MB kidogo sana zinazotumika. Inatumia 3G, 4G na Wi-Fi internet kusikiliza radio.


5. Ina size ndogo sana ambayo ni rahisi kuidownload kwenye simu.

No comments:

Powered by Blogger.