LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAANDAMANO YA WANANCHI MKOANI GEITA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Wanakijiji wa Kijiji Cha Hililika Kata ya Nyarugusu wakiandamana kuelekea kwenye eneo ambalo mwekezaji anajenga kiwanda kwaajili ya shughuli za uchinjuaji wa Dhahabu.

Wanakijiji wakishirikiana kuziba Eneo la Bara bara ya kuelekea kwenye kiwanja ambapo ndiko ujenzi unaendelea.


Wakinamama wa Kijiji wakishiriki maandamano ya kupinga ujenzi wa Kiwanda cha Uchenjuaji Kijijini Hapo.

Kisima cha Kijiji ambacho kinategemewa na wananchi ambacho ndicho ambacho wamelalamikiwa uwezekano wa maji yake kuharibika kutokana na shughuli za madini.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Hililika Bw,Daniel Mwigulu Nkela  ambaye analalamikiwa na wananchi kukubaliana na mwekezaji kwenye eneo hilo bila ya kuwashirikisha akizungumza na wananchi juu ya uwamuzi huo ambao ulifanyika

Wananchi wakizidi kuonesha msimamo wao wa kutokukubalinana na kile ambacho Mwenyekiti alikisema.

Moja kati ya wananchi wa kijiji cha Hililika akizungumzia uwamuzi wao wa kuandamana.



Bwawa la Maji la Kunyweshea mifugo likiwa kwenye eneo ambalo ni karibu na sehemu ya Kiwanda cha kuchenjulia Dhahabu.




Wananchi wa Kijiji cha Hililika Kata ya Nyarugusu Wilaya na Mkoa wa Geita jana wameandamana kupinga mwekezaji kuweka kiwanda cha kuchenjulia Dhahabu kwa madai kuwa chanzo cha maji ambacho wanakitegemea kijijini hapo kipo karibu na planti ambayo inajengwa na kwamba inaweza kusababisha madhara ya afya kutokana na Kemikali yaCyanide  ambayo hutumika kwenye shughuli za uchenjuaji.

Wakizungumza na mtandao wa maduka online kwa vipindi Tofauti wamesema kuwa hofu kubwa waliyonayo ni kutokana na sumu  ya kuchenjulia dhahabu kwani ni hatari kwa afya zao na viumbe ambavyo vinazunguka maeneo ambayo wanafanyia kazi.

“Sehemu hii ni karibu sana na eneo ambalo tunachotea maji sasa kama wakiweka hicho kiwanda sisi wananchi tutakuwa kwenye hali gani hebu serikali ijaribu kulitazama swala hili kwa umakini zaidi tutaisha kutokana na sumu ya kuozesha marudio”Alisema Bi,Hellen Mbaru.

“Sawa eneo hili ni la mtu Binafisi na lipo ndani ya kijiji cha Hililika na kwamba tunaambiwa kuwa watawapa angalizo wawekezaji ndani ya mwaka mmoja endapo kama kuna maafa ambayo yatajitokeza watawafukuza kweli na hali hii jamani hadi watu wadhurike ndio tahadhili ichukuliwe mimi naomba sana serikali ilitazame hili”Alisema

Hata hivyo Lawama nyingi zimemwangukia Mwenyekiti wa Kijiji kuwa amehusika kwa kiasi kikubwa Kwa kuchukua rushwa kutoka kwa mwekezaji na kwamba kwa sasa hawana imani naye hali ambayo imesababisha kufunga ofisi ya Kijiji.

Kutokana na hali hii askari Polisi wamefika kwenye eneo hilo na kumshauri Mwenyekiti wa Kijiji hicho ambaye alifika kwenye eneo hilo kuona umuhimu wa kuwasikiliza wananchi na kusitisha ujenzi wa Planti hiyo.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kijiji hicho Daniel Mwigulu Nkela,amesema kuwa maamuzi ambayo yalichukuliwa hayakuwa ya peke yake bali ni ya wajumbe wote ambao waliridhia eneo hilo.

“Maana ya serikali kuna wajumbe 25 mimi kama mwenyekiti sina mamlaka ya kuidhinisha eneo hili peke yangu mwekezaji anapotaka kuingia tunaitisha serikali ya kijiji inakaa na inapokaa kuna kuwa na mahojiano kati ya mwekezaji na wajumbe wa  serikali ya kijiji mimi kazi yangu ni kulinda maadhimio kikao tu sina mamlaka ya kuhidhinisha eneo lolote lile”Alisema Mwigulu.

Maduka online imemtafuta mwekezaji wa eneo hilo kutaka kujua makubaliano yake na serikali ya kijiji ambapo moja kati ya wasimamizi wa eneo  wamegoma kuzungumzia swala hilo na kwamba anaye weza kuzungumzia swala hilo ni meneja wao ambaye yupo Mwanza kwa sasa hata hivyo jitihada bado zinaendelea kujua makubaliano yalikuwaje.


IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE

No comments:

Powered by Blogger.