LIVE STREAM ADS

Header Ads

UMISSETA MKOA WA DAR ES SALAAM YAPAMBA MOTO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Kaimu Katibu Tawala upande wa Uchumi na Uzalisha Mkoa wa Dar es salaam Ndg Edward Otieno akizungumza wakati wa ufunguzi wa  UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam jana Mei 28, 2017 katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwasalimu wanamichezo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam 
Baadhi ya wanamichezo kutoka Manispaa za Mkoa wa Dar es salaam wakifatilia mchezo kati ya Ilala na Ubungo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisalimiana na mchezaji wa Mpira wa Miguu Manispaa  ya Ubungo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam jana katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kushoto), Kaimu Katibu Tawala upande wa Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dar es salaam Ndg Edward Otieno (Katikati) na Afisa Elimu Mkoa wa Dar es salaam Khamisi Lissu wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa hamasa kwa timu ya UMISSETA Wilaya ya Ubungo wakati wa ufunguzi wa  UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiimba wimbo maalumu wa Michezo ya UMISSETA wakati wa ufunguzi wa  UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam.

Na Mathias Canal, Dar es salaam
Maandalizi ya ngazi ya Mkoa wa Dar es salaam Kwa Mashindano ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania yamezidi kupamba Moto katika Uwanja wa Uhuru na Uwanja wa Taifa Jjijini Dar es salaam.

Maandalizi hayo kwa ngazi ya Mkoa kwa ajili ya kupata timu ya mkoa wa Dar es salaam yalianza  jana Mei 28, 2017 Kwa kuhusisha Manispaa za mkoa wa Dar es salaam ikiwemo Manispaa ya Ilala, Temeke, Kinondoni, Kgamboni na Ubungo.

Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo kwa ngazi ya Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam Kaimu Katibu Tawala katika upande wa Uchumi na Uzalisha Mkoa wa Dar es salaam Ndg Edward Otieno aliwasihi washiriki kutumia weledi wao wa mafunzo waliyoyapata kuhusu michezo na kuonyesha umahiri wao ili kuchaguliwa katika timu ya Mkoa.

Wanafunzi hao ambao wameweka kambi katika Shule ya Sekondari Jitegemee mpaka Mei 31, 2017 wataanza safari ya kuelekea Jijini Mwanza kwa ajili ya mashindano hayo ngazi ya Taifa yanayotaraji kuanza kufanyika katika uwanja wa CCM Kirumba June 6, 2017.

Otieno alisema kuwa vijana hao wanapaswa kutambua kuwa michezo ndio ajira inayolipa zaidi duniani hivyo wanapaswa kudumisha nidhamu kwa kipindi chote Cha mashindano.
Aliongeza kuwa wanapaswa kutambua kuwa timu zote za Mkoa wa Dar es salaam zitakwenda Mwanza kushindana katika michezo hiyo ngazi ya Taifa na si kushiriki pekee.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo aliyezuru katika Uwanja wa Uhuru kujionea Timu ya Vijana wake kutoka Manispaa ya Ubungo ikichuana vikali na timu ya Manispaa ya Ilala alipongeza juhudi za washiriki wote ambao wameonyesha nidhamu ya Hali ya juu.

"Ukiona vijana Wana nidhamu Kama hivi ni vyena kuwapongeza na kuwatia moyo maana Bado Wana safari ndefu kimichezo na kimaisha" Alisema MD Kayombo.

Mkurugenzi Kayombo alitilia msisitizo zaidi kutumia weledi wao ili kurejesha heshima ya michezo katika Manispaa ya Ubungo na Mkoa wa Dar es salaam Kwa ujumla.

No comments:

Powered by Blogger.