LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZIRI MWAKYEMBE AWAHIMIZA WAANDISHI WA HABARI KUJIKITA KWENYE HABARI ZA UCHUNGUZI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habaru Duniani, jana Mei 03,2017, kitaifa Jijini Mwanza. Waziri Dkt.Mwakyembe alimwakilisha Rasi John Pombe Magufuli.

Dkt.Mwakyembe aliwaasa waandishi wa habari kuwa na weledi kwenye utendaji wao wa kazi ikiwemo kujikita kwenye habari za uchunguzi wa kina na siyo hisia alizosema atazilinda na kuzitetea huku akiwahimiza wahariri nchini kuwa na utaratibu wa kukutana na Mkurugenzi wa Habari Maelezo japo mara moja kwa mwezi ili kujadiliana kwa pamoja mafanikio na changamoto za utendaji kazi kwenye tasnia ya habari kwa manufaa ya taifa.

Aidha alionesha utayari wa kufungua milango ya majadiliano kuhusiana na sheria mpya ya vyombo vya habari nchini hususani katika baadhi ya vipengele vinavyolalamikiwa na wanahabari akisema sheria hiyo haijaandikwa kwenye mawe, ishara tosha kwamba kukiwa na mazungumzo, mabadiliko katika sheria hiyo yanaweza kufanyika.
BMGHabari
Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Salome Kitomari, akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habaru Duniani, jana Mei 03,2017, kitaifa Jijini Mwanza.

Kitomari alibainisha kuwa takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya waandishi wa habari 100 kote duniani waliuawa mwaka 2016kutokana na majukumu yao ya kazi huku pia kukiwa na matukio ya upigwaji na utekaji wa waandishi wa habari ambapo kwa Tanzania zaidi ya kesi 30 za manyanyaso na ukiukwaji wa uhuru wa vyombo vya habari ziliripotiwa.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Fikra Makini, Nyakati za Changamoto, Jukumu la Vyombo vya Habari katika kudumisha Amani, Usawa na Jamii Jumuishi".
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO nchini Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mwakilishi mkazi wa taasisi ya FES nchini Tanzania, Michael Schulteiss, akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Kitaifa Jijini Mwanza jana.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakfu wa Vyombo vya Habari nchini (TMF), Ernest Sungura, akizungumza kwenye maadhimisho hayo
Mwakilishi wa balozi wa Marekani nchini Tanzania, Virginia Blaser akizungumza kwenye maadhimisho hayo
Mwakilisho wa balozi za Ulaya kutoka Sweeden, akizungumza kwenye maadhimisho hayo
Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini, Deogratius Nsokolo, akizungumza kwenye maadhimisho hayo
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez, akizungumza kwenye maadhimisho hayo
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini TEF, Theophil Makunga, akizungumza kwenye maadhimisho hayo
Valerie Msoka kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini Tanzania TAMWA, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mama Pili Mtambalike akizungumza kwa niaba Mkurugenzi wa TCRA kwenye maadhimisho hayo
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd, Francis Nanai akizungumza kwa niaba ya wamiliki wa vyombo vya habari nchini MOAT
Mwanataaluma ya habari mkongwe nchini, Salim Said Salim akizungumza kwa niaba ya wengine wengine kwenye maadhimisho hayo
Mtaalamu wa Mawasiliano nchini, Innocent Mungy, akisherehesha maadhimisho hayo
Viongozi mbalimbali meza kuu
Baadhi ya washiriki kwenye maadhimisho hayo ambapo kushoto ni Mkurugenzi wa Metro Fm Mwanza, Amran Batenga.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe, akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini TEF, Theophil Makunga (kulia).
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia) akiwa na Mwakilishi wa balozi wa Marekani nchini Tanzania, Virginia Blaser (kushoto), wakati akiwasili kwenye maadhimisho hayo
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe na viongozi mbalimbali wakishuhudia mchezo wa kucheza na nyoka kutoka kikundi cha ngoma za asili cha Bujora.

No comments:

Powered by Blogger.