LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAMLAKA YA MAJI SAFI MKOANI SHINYANGA YAKUTANA NA WADAU WAKE.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) imekutana na wadau wa huduma ya maji kujadili rasmu ya mkataba wa huduma kwa wateja ambapo mkataba utakaopitishwa na wadau utaanza kutumika kuanzia Julai Mosi mwaka huu.

Warsha ya kujadili mkataba wa huduma kwa wateja imefanyika leo katika ukumbi wa Vijana Center Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro.

Akizungumza katika warsha hiyo,Matiro aliwataka wadau wa maji kujadili rasmu hiyo kwa umakini zaidi ili kuweka mambo ya msingi ambayo yatapunguza malalamiko kutoka wateja ikiwemo ongezeko la bei ya maji kwa watumiaji wa majumbani.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Reuben Mwandumbya alisema kutokana mamlaka hiyo kuwajali wateja wake imeona ni vyema kukutana na wadau ili kujadili mkataba mpya wa huduma kwa wateja.

“Mkataba uliokuwepo umemaliza muda wake hivyo tumeleta kwenu rasmu ya mkataba ili tujadili kwa pamoja tuweze kuboresha zaidi huduma ya maji kwa wateja wetu”,alieleza Marco.

Miongoni mwa wadau walioshiriki katika warsha hiyo ni meya wa manispaa ya Shinyanga,madiwani,viongozi wa dini,viongozi wa taasisi mbalimbali,watendaji wa kata,wenyeviti wa serikali za mitaa,waandishi wa habari na wadau mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufungua warsha/kikao cha kujadili rasmu ya huduma kwa wateja 
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akizungumza katika warsha hiyo.Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla,kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Reuben Mwandumbya
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga ,Josephine Matiro akizungumza katika warsha ya wadau wa maji manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga ,Josephine Matiro akisisitiza jambo katika warsha hiyo
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Reuben Mwandumbya akielezea umuhimu wa wadau wa maji kujadili rasmu ya mkataba wa huduma kwa wateja
Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla akizungumza ukumbini
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Agnes Machiya akizungumza katika warsha hiyo
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Agnes Machiya akizungumza
Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard akielezea kuhusu mkataba wa huduma kwa wateja
Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard akiendelea kuelezea kuhusu mkataba wa huduma kwa wateja
Afisa Rasilimaliwatu na Utawala wa SHUWASA,Kambira Mtebe akifafanua kuhusu mktaba wa huduma kwa wateja
Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii manispaa ya Shinyanga,Hassan Mwendapole akiongoza majadiliano wakati wa warsha hiyo
Warsha inaendelea
Warsha inaendelea
Diwani wa kata ya Ndembezi (CCM) David Nkulila akichangia hoja katika warsha hiyo
Diwani wa viti maalum kata ya Shinyanga Mjini,Zenna Gulam (Chadema) akichangia hoja
Mchungaji Obeid Jilala ambaye pia ni diwani wa kata ya Lubaga (Chadema) akichangia hoja ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Warsha inaendelea
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wadau wakiwa ukumbini
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

No comments:

Powered by Blogger.