MABATINI STAR YAENDELEA KUTOA DOZI NDONDO CUP 2017 JIJINI MWANZA
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Judith Ferdinand, Mwanza
Timu ya
Mabatini Star yaendelea kutoa kichapo baada ya kuifunga Nyegezi Terminal goli
3-2, katika mashindano ya Ndondo Cup yanayoendelea kutimua vumbi kwenye uwanja wa kisasa na mkongwe wa
Nyamagana jijini hapa.
Katika
mchezo huo ambao ni wa raundi ya pili hatua ya makundi ilizikutanisha timu za
kundi B, ambapo kipindi cha kwanza kila timu ilijitahidi kushambulia lakini
juhudi hizo hazikuzaa matunda mpaka mapumziko matokeo yalikua bila bila.
Katika
kipindi cha pili timu zote zilifanikiwa kutikisa nyavu za mwenzie ambapo Mabatini Star ilifunga magoli
3 kupitia mshambuliaji wake Kanichi Andrew dakika ya 47,54 na 65 huku Nyegezi
Terminal wakipata goli dakika ya 53 kupitia mshambuliaji wake Ramadhani Mandinda
na Twalibu Ally aliyefunga dakika ya 76.
Hata hivyo
Kanichi Andrew ndiye aliyeibuka mchezaji bora wa mchezo huo na kufanikiwa
kupatiwa zawadi ya shilingi 30000 kutoka kwa
Hasafu Barber Shop kupitia
Mkurugenzi wake Hamis Swahibu ambae amekua akiendelea kutoa zawadi kwa ajili ya
kuwahamasisha wachezaji kufanya vizuri.
Kanichi
alisema, siri ya ushindi ni
kujituma,mazoezi,kufuata maelekezo ya kocha,uwezo na jitihada binafsi za
wachezaji.
Naye Kocha
wa Mabatini Star Omar Bakar
alisema,mechi ilikua ngumu ila wanamshukuru Mungu wameweza kuibuka na ushindi.
Kwa upande
wake Kocha wa Nyegezi Terminal Ibrahim Mlumba alisema, mechi ilikua ngumu,na
sababu ya kupoteza mchezo huo ni kutokana na mabeki wa timu hiyo kutokua
makini,hivyo wanajipanga ili mchezo ujao waweze kufanya vizuri.
Aidha timu
zote mbili katika raundi ya kwanza ya hatua ya makundi ya mashindano hayo
ziliweza kushinda ambapo Nyegezi Terminal ilishinda goli 1-0 dhidi ya Buzuruga
Terminal huku Mabatini Star ikifunga goli 6 -3 dhidi ya Igoma Heroes.
Wakati huo
huo katika mchezo wa kwanza timu ya
Iseni Fc iliibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Viva Fc.
Timu ya
Iseni Fc ilifunga magoli kupitia washambuliaji wake Khatibu Abdallah dakika ya
2, Paul Godfrey dakika ya 61 na Juma Salige dakika ya 80, huku VIVa Fc
wakifunga kupitia Ballo Kashind dakika ya 33 na Emma Kijeshi dakika ya 46.
Juma Salige
ndiye aliibuka mchezaji bora katika mchezo huo na kupatiwa kitita cha shilingi
30000.
No comments: