SHIRIKA LA KIVULINI LATOA MAFUNZO SHINYANGA VIJIJINI
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Afisa Mradi kutoka shirika la Oxfam,Mkamiti Mgawe akifungua mafunzo ya usawa wa kijinsia,sera na sheria zinazohusu usawa wa kijinsia kwa wadau wanaotekeleza mradi wa “Usawa wa kijinsia kiuchumi kwa wanawake na vijana”.
Shirika la
Kivulini limetoa mafunzo ya usawa wa kijinsia,sera na sheria zinazohusu usawa
wa kijinsia kwa wadau wanaotekeleza mradi wa “Usawa wa kijinsia kiuchumi kwa
wanawake na vijana” kutoka kata ya Nyida,Nsalala na Itwangi katika halmashauri
ya wilaya ya Shinyanga.
Mradi huo unatekelezwa
na Shirika la OXFAM kwa kushirikiana na shirika la Kivulini. Mafunzo hayo ya
siku moja yamefanyika leo Alhamis Septemba 28,2017 katika ukumbi wa Empire
Hotel mjini Shinyanga.
Miongoni mwa
wadau waliofaidika na mafunzo hayo ni maafisa maendeleo ya jamii,maafisa
watendaji wa vijiji na kata,viongozi wa mabaraza ya kata,sungusungu,maafisa
ustawi wa jamii,afya,wawakilishi kutoka dawati la jinsia wilaya ya Shinyanga.
Awali
akizungumza katika mafunzo hayo, Ofisa mradi kutoka Shirika la Kivulini lenye
makao makuu yake jijini Mwanza, Eunice Mayengela alisema lengo la mafunzo hayo
ni kuwajengea uelewa viongozi wa serikali za mitaa kuhusu masuala ya usawa wa
kijinsia,sera na sheria zinazohusu usawa wa kijinsia.
“Tunatekeleza
mradi wa “usawa wa kijinsia kiuchumi kwa wanawake na vijana katika halmashauri
ya wilaya ya Kishapu na Shinyanga Vijijini na leo tumekutana na wadau kutoka
kata tatu za Nyida,Nsalala na Itwangi za Shinyanga Vijijini,lengo la mradi huu
ni kujenga uwezo, uelewa na mikakati ya kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuzuia
na kupambana na ukatili wa kijinsia”,aliongeza Mayengela.
Akizungumza
wakati wa kufungua mafunzo hayo,mgeni rasmi ambaye ni Afisa Mradi kutoka
shirika la Oxfam,Mkamiti Mgawe alisema mafunzo hayo yatawasaidia wadau hao
kutekeleza vyema majukumu yao katika kupinga na kupambana na ukatili wa
kijinsia kwenye maeneo yao.
“Mafunzo
haya yanajumuisha viongozi wa serikali za mitaa ambako ndiko matukio mengi ya
ukatili wa kijinsia yanafanyika,tumieni elimu hii kufikisha ujumbe kwa jamii
kwamba ukatili wa kijinsia haukubaliki”,alisema Mgawe.
Alisema
viongozi wa serikali za mitaa na maafisa ustawi wa jamii wana jukumu la
kuwashauri waathirika wa vitendo vya kikatili juu ya haki zao kupeleka mashtaka
ya ukatili katika vyombo vya usalama ikiwemo polisi na mahakama.
Naye
Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Glory Mlaky alizitaja baadhi ya sababu za ukatili
katika jamii kuwa ni wanawake wengi kuamini kuwa wao ni dhaifu,wanaohitaji
kuongozwa,kuelekezwa na kuwajibishwa na wanaume pamoja na wanawake hao kukosa
elimu kuhusu haki zao.
Kwa upande
wake,Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana Halmashauri ya wilaya
ya Shinyanga vijijini,Deus Masili Muhoja aliwasihi viongozi wa serikali za
mitaa kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia na
kuwasisitiza wawe tayari kutoa ushahidi ili waathirika wapate haki yao.
Afisa kutoka
Jeshi la Polisi wilaya ya Shinyanga,Joseph Christopher aliwataka viongozi wa
jeshi la jadi sungusungu kuimarisha usalama katika maeneo yao na wanapokamata
mhalifu wamfikishe kituo cha polisi badala ya kujichukulia sheria mkononi
kumwadhibu.
Afisa Mradi kutoka shirika la Oxfam,Mkamiti Mgawe akifungua mafunzo ya usawa wa kijinsia,sera na sheria zinazohusu usawa wa kijinsia akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini
Afisa Mradi kutoka shirika la Oxfam,Mkamiti Mgawe akizungumza ukumbini
Wadau wakifuatilia mafunzo
Afisa mradi wa kutoka Shirika la Kivulini,Eunice Mayengela akisisitiza jambo ukumbini.
Mafunzo yanaendelea....
Afisa mradi wa kutoka Shirika la Kivulini,Eunice Mayengela akizungumza ukumbini.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Glory Mlaky akitoa elimu kuhusu masuala ya ukatili katika jamii.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Glory Mlaky akielezea kuhusu ukatili wa kingono.
Bwana Beatu Berenardo kutoka kijiji cha Welezo kata ya Nsalala akichangia hoja ukumbini
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Afisa Mtendaji wa kata ya Nyida Daudi Lazaro akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Glory Mlaky akiendelea kutoa mada wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia mada ukumbini
Mwenyekiti wa Baraza la ardhi kutoka kata ya Itwangi,Joseph Maganga akichangia hoja ukumbini
Washiriki wa mafunzo wakifanya kazi ya kundi
Kazi za makundi zinaendelea
Kazi ya kundi inaendelea
Afisa Maendeleo wa kata ya Nsalala,Beatrice Macha akiwasilisha kazi ya kundi lake
Katibu wa jeshi la sungusungu kata ya Nsalala John Machiya akiwasilisha kazi ya kundi lake
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Mwakilishi wa Jeshi la Polisi wilaya ya Shinyanga,Joseph Christopher akizungumza ukumbini
Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini,Deus Masili Muhoja akizungumza ukumbini
Picha ya pamoja washiriki wa mafunzo hayo.
Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
No comments: