LIVE STREAM ADS

Header Ads

Alliance FC yaichapa Pamba FC ligi daraja la kwanza

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Judith Ferdinand, Mwanza
Timu ya Alliance FC imeichapa Pamba FC,goli 2-1, katika mchezo wa ligi daraja la kwanza nchini  msimu wa 2017/2018.

Mchezo huo uliochezwa jana katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, ambapo Pamba FC wakiwa wenyeji.

Timu ya Alliance FC walifunga goli  kupitia washambuliaji wake  Shaban William dakika ya 33 na Dickson Ambundo dakika ya 52 huku Pamba FC wakipata goli dakika ya 73 kupitia Severine Faustine.

Katika mchezo huo dakika ya 89 mchezaji wa  Pamba FC Yunus Manota alipewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi kipa wa Alliance FC.

Naye Kocha Msaidizi wa Alliance FC Kessy Mziray alisema, anamshukuru Mungu kwa kushinda na kupata pointi tatu,kwani mechi hiyo ilikua ni ngumu, pia aliwapongeza vijana kwa kuzingatia nidhamu na walivyoelekezwa.

Kwa upande wake Kocha wa  Makipa wa  Pamba FC  Emmanuel Kingu alisema, kushindwa siyo miujiza bali ndivyo mchezo wa mpira ulivyo,hivyo  wanajipanga na wanaamini watashinda na kupata pointi tatu katika uwanja huo wa Nyamagana.

No comments:

Powered by Blogger.