LIVE STREAM ADS

Header Ads

Maridhiano ya Makinikia yawagusa watoto wafanyakazi wa nyumbani Jijini Mwanza

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Binagi Media Group
Watanzania wengi wamefurahishwa na maridhiano baina ya serikali ya Tanzania na kampuni ya Barrick yaliyofikia tamati jana Oktoba 19,2017 Ikulu Jijini Dar es salaa.

Mambo kadhaa yaliyoridhiwa ni pamoja na kampuni Barrick kukubali masharti ya uendeshaji wa wa shughuli za uchimbaji wa madini nchini, ofisi zake za Afrika Kusini kuhamishiwa nchini pamoja na pande zote mbili kugawana faida sawa ya 50/50 kwenye uzalishaji wa madini.

Pia kampuni ya Barrick kukubali kuilipa serikali ya Tanzania dolla Milioni 300 takribani shilingi bilioni 700 kama sehemu ya fidia ya makosa kadhaa ya kibiashara yaliyofanywa na kampuni tanzu za Barrick hapa nchini.

Suala hilo la maridhiano limewagusa hadi watoto wafanyakazi wa nyumbani chini ya Shirika la WoteSawa ambapo kabla ya kuanza semina yao hii leo, wamezungumzia suala la maridhiano ya makinikia wakitana nao kama watoto wanufaike na rasilimali zilizopo nchini.

Watoto hao kutoka Kata mbalimbali Jijini Mwanza ikiwemo Mkuyuni, Isamilo, Igogo, Buhongwa na Mkolani wamekutana ili kujadili changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo utumikishwaji, ukatili, kujiepusha na mimba za utotozi na namna ya kupambana nazo.

Baadhi ya watoto hao wameomba kusaidia kimasomo ili waweze kutimiza ndoto zao na siyo kuishia kufanya kazi za nyumbani.
Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WOTESAWA, akizungumza kwenye semina hiyo
Afisa Miradi akizungumza kwenye semina hiyo
Baadhi watoto wafanyakazi wa nyumbani waliohudhuria semina hiyo. 
Miongoni mwa watoto hao wameomba kusaidia kimasomo ili waweze kutimiza ndoto zao na siyo kuishia kufanya kazi za nyumbani.
Rais John Pombe Magufuli akishuhudia Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corp. Profesa John Thornton (wa pili kulia) na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi (wa pili kushoto) wakitia sahihi ripoti ya makubaliano ya biashara ya madini, katika hafla iliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Afisa Uendeshaji wa kampuni hiyo, Richardc William. Picha na Ikulu

No comments:

Powered by Blogger.