LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jogoo la shamba lawika mjini michuano ya Ndondo Cup 2017 Jijini Mwanza

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Judith Ferdinand, Mwanza
Hatimaye jogoo la shamba limewika mjini, baada ya timu ya Morning Star kutoka Kisesa Wilayani Magu nje kidogo ya Jiji la Mwanza, kuibana mbavu Mabatini Star kwa goli 5-1.

Morning Star ilitoa kichapo hicho jana katika mchezo wa  kumtafuta mshindi wa  tatu wa  mashindano ya Ndondo Cup 2017 yanayorindima kwenye uwanja wa  Nyamagana jijini Mwanza.

Katika mchezo huo Morning Star walionekana kushambulia zaidi ambapo juhudi hizo zilizaaa matunda na kufunga magoli kupitia washambuliaji wake John Buguba dakika ya 9 na 35, Malulu Thomas dakika 25 na 75 huku Juma Masinde akipatia timu hiyo goli la 5  dakika 89.

Mabatini Star walifunga goli dakika ya 76  kupitia Frank Kulwa huku dakika ya 79  mchezaji wa timu hiyo  Rashidi Shaibu alipewa kadi nyekundu baada ya kutoa lugha chafu akiwa uwanjani.

Akizungumzia mchezo huo kocha wa Morning Star Wilbert Mwita alisema, anamshukuru Mungu kwa kuitimisha mchezo wa mwisho  huku wakiibuka na ushindi, aliwapongeza Clouds kwa kuanda mashindano hayo ambayo yanasapoti vipaji vya vijana sambamba na  kuvikaribisha vilabu vya soka  kuwasajii wachezaji wa timu hiyo kwani wapo sokoni na wanajiandaa na msimu ujao.

Kwa upande wake Nahodha wa Mabatini star Frank Kulwa alisema, mchezo ndivyo ulivyo na wanajipanga na msimu ujao ambao  kalenda imesogezwa mbele, pia aliwapongeza waandaaji kwa kuleta mashindano hayo Mwanza ambayo yamekuwa na ushindani mkubwa na vijana wamepata sehemu ya kuonyesha vipaji vyao, sambamba na kuwataka mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuiunga mkono ili iweze kufanya vizuri zaidi katika mashindano mengine.

John Buguba kutoka Morning Star ndiye aliyeibuka mchezaji bora wa mechi hiyo na kujinyakulia kitita cha shilingi 30000 kutoka kwa HASFU Barber Shop.

No comments:

Powered by Blogger.