LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mamilioni ya shilingi kuwaniwa kwenye mbio za Rock City Marathon 2017

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Judith Ferdinand, Mwanza
Zaidi ya shilingi Milioni 40 za kitanzania zinatarajiwa kushindaniwa katika mashindano ya mbio za Rock City Marathon 2017, zinazotimua vumbi Oktoba 29 mwaka huu katika viunga mbalimbali vya Jiji la Mwanza na kutamatikia katika uwanja wa  CCM Kirumba.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuwa na washiriki wa ndani na nje ya nchini ikiwemo kutoka Kenya, Uganda, Ethiopia, Sudan ya Kusini, Marekani na China.

Kutakuwa na makundi matano, kundi la kwanza ni umbali wa km 42, la pili km 21, la tatu km tano, la nne km tatu huku la tano likiwa la mita 100, 200, 400, 800 na 1500.

Hayo yalisemwa na Bidan Lugoe ambaye ni mratibu wa mashindano hayo yanayoandaliwa na kampuni ya Capital  Plus International, yakilenga kuendeleza mchezo wa riadha pamoja na kuutangaza utalii.

Alisema mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa mara ya nane mfululizo awali yalikua yakifanyika kwa km 21 "half marathon", ingwa kwa mwaka huu yameboreshwa zaidi na yatakuwa na urefu wa km 42 "full marathon".

Jumla ya milioni 40 zitatolewa kama zawadi katika mashindano haya, ambapo mshindi  wa kike na kiume kila mmoja atapatiwa zawadi ambapo wa kwanza kwa mbio za km 42 atapata milioni nne, wa pili milioni mbili, wa tatu milioni moja na km 21 wa kwanza atajinyakulia milioni mbli, wa pili milioni moja na watatu laki tano.

Kwa upande wa km tano ambapo watashiriki watu wenye ualibino, mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shilingi 150,000, wa pili 100,000 na wa tatu 50,000 ikiwa ni njia ya kupinga  mauaji ya watu hao, ambapo pia kutakua na zawadi kwa mbio za ndani ya uwanja za mita 100, 200, 400, 800 na 1,500 kwa wanafunzi  wa shule za  msingi na sekondari ikiwa ni kukuza mchezo wa riadha.

Lugoe Alisema hadi sasa zaidi ya washiriki 500 wa  ndani ya nchini na 70 kutoka nje nchini wameisha jisajili na kwamba usajili bado unaendelea hivyo matarajio ni kuwa na washiriki kati ya 4000 na 5,000 katika mbio hizo.

Mbio hizo zitaanza majira ya saa 12 asubuhi hadi 12 jioni siku ya jumamosi Oktoba 29 yakianzia na kutamatikia uwanja wa CCM Kirumba ambapo pia itakuwa ni fursa kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na viunga vyake kukutana ili kujionea mbio hizo ikiwa ni sehemu ya burudani pia.

No comments:

Powered by Blogger.