LIVE STREAM ADS

Header Ads

Milo Clan Watoto wa Muji wafuzu fainali ya Ndondo Cup 2017 Jijini Mwanza

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Judith Ferdinand, Mwanza
Hatimaye hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Ndondo Cup 2017 Jijini Mwanza imemalizika kwa timu ya Milo Clan (Watoto wa Muji), kufuzu fainali baada ya kuilaza timu ya Morning Star kwa goli 1-0.

Katika mchezo huo uliopigwa jana kwenye dimba la Nyamagana, hadi mapumziko hakuna timu ambayo iliweza kuliona lango la mwenzie.

Kipindi cha pili Milo Clan ilifunga goli dakika ya 56 kupitia kwa mshambuliaji wake Karim Said, goli ambalo liliipatia timu hiyo ushindi.

Kocha wa timu ya Milo Clan, Hussein Tade alisema mchezo kwao ulikua mgumu ingawa anamshukuru Mungu kwa kuibuka na ushindi huo, hivyo  atafanya marekebisho safu ya kati ili aibuke na ushindi kwenye mchezo wa fainali na hatimaye kuibuka mabingwa wa mashindano hayo ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika Jijini Mwanza.

Naye Kocha wa timu ya Morning Star, Wilbert  Mwita alisema mchezo huo ulikua mzuri na kwamba walicheza wake walicheza kiufundi ingawa hawakupata nafasi kuzifumania nyavu hivyo anaelekeza nguvu zote kwenye mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu.

Mchezaji Malulu Thomas kutoka timu ya Morning Star aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo na kujinyakulia kitita cha shilingi 30,000 kutoka kwa HASFU Barber Shop ambao ni miongoni mwa wadau wa Ndondo Cup Jijini Mwanza.


Mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu utapigwa kesho Oktoba 26 ambapo timu za Mabatini Star pamoja na Morning Star zitachuana huku fainali ikipigwa ijumaa Oktoba 27 mwaka huu kati ya timu ya Milo Clan na Mnadani Fc, michezo yote ikipigwa kwenye dimba la Nyamagana majira ya saa kumi alasiri.

No comments:

Powered by Blogger.