LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mgomo wa daladala za Buhongwa-Misungwi mkoani Mwanza wanukia

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Na Oscar Mihayo, Mwanza
Madereva na Makondakta wa daladala zinazofanya safari zake kati ya Buhongwa Jijini Mwanza na Misungwi wameilalamikia halmashauri ya Misungwi kwa kushindwa kuwawekea vituo vya kushusha na kubeba abiria katika barabara hiyo hatua ambayo imeongeza kasi ya wao kukamatwa na askari wa jeshi la polisi, kitengo cha usalama barabarani.

Madereva hao wanasema kutoka Buhongwa hadi hadi Misungwi kuna vituo vitano tu huku vikiwa na umbali mrefu kati ya kituo kimoja na kingine hatua inayosababisha kuzozana kila siku na abiria pindi wanaposhindwa kuwashusha katika eneo ambalo hakuna kituo.

"Tunapigwa na abiria ama wakati mwingine tunanyimwa nauli zetu kutokana na kuwapitilia eneo la makazi yao na wakati huo tukionyesha usamalia wema na kuwashusha, polisi wanatukamata na kututoza faini kubwa hadi shilingi 60,000". Alisema Issa Burwa.

Walisema ni muda mwafaka sasa wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi kukaa meza moja na wadau wa usafirishaji pamoja na watu wa usalama barabarani ili kujadili changamoto hiyo kabla hawajaitisha mgomo utakoathiri shughuli za wananchi.
Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Kanda ya Ziwa, Dede Petro alitoa rai kwa almashauri hiyo kuhakikisha inatatua changamoto hiyo kabla mgomo wa daladala hizo haujatokea na hivyo kuathiri shughuli za uzalishaji kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

"Halmashauri tunaomba mtusikilize sisi, Rais wetu Dkt.John Magufuli kama raia namba moja nchini anapenda kuona wanyonge wanaishi vyema katika nchi hii, sasa msije mkatufanya tufanye kitu cha kupingana na Rais wetu, tunataka maridhiano yafanyike haraka kabla jahazi halijaenda mrama". alisema Petro.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Misungwi, Itendele Maduhu anakiri uwepo wa chanagamoto hiyo na kuahidi kuishughulikia ndani ya wiki moja baada ya kukutana na wa pande zote ili kujadiliana kwa kina.


“Ni kweli jamani tunakubali uwepo wa changamoto hiyo, na niwaahidi kuweni wapole wakati suala hili tukilitafutia ufumbuzi ili mambo yaende sawa na nina imani tatizo hili litaisha". Alisema Maduhu.

No comments:

Powered by Blogger.