LIVE STREAM ADS

Header Ads

Taasisi ya KCRBP yajitosa vita dhidi ya ukatili kwa watu wenye ualibino

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Picha kutoka maktaba, Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye ualibino mkoani Mwanza akizungumza kwenye moja ya hafla zilizowahi kufanyika mkoani humo.

Judith Ferdinand,Kishapu
Asasi ya ya kijamii ya Karagwe Community Based Rehabilitation Programs (KCRBP) imejizatiti kutoa elimu ya utambuzi katika jamii kuhusu masuala ya ualibino (Albinism), kupitia mradi wake jumuishi wa watu wenye ualibino

Meneja Mradi wa taasisi hiyo, Florence Rugemalira aliyasema hayo wakati akizungumza na BMG alipotembelea wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

Alisema asas hiyo itaendelea kuelemisha jamii kuhusu kutambua watu wenye ualbino kwani lengo la  mradi huo ni kuvunja dhana potofu iliyojengeka katika jamii kuhusu kundi hilo.

Pia  alisema mradi huo ambao ulianza Agosti mwaka huu utatekelezwa katika mikoa mitano ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Simiyu, Geita, Shinyanga na Kagera ambapo shirika hilo litatoa elimu zaidi kuhusiana na mambo ya watu wenye ualbino ili kuwanusuru na ukatili kutokana na dhana potofu juu ya ualibino.

Rugemalira aliwasihi wanajamii kuacha kuwatenga na kuwatendea ukatili watu wenye ualbino na badala yake wawashirikishe katika shughuli za kimaendeleo katika jamii.

Naye Katibu Mkuu wa asasi watu wenye Ualbino (TAS) wilayani  Kishapu, Seif Rashid aliiomba serikali kuendelea kusaidia kutokomeza tatizo unyanyasaji, ukatili na ukataji wa viungo kwa watu wenye ualibino ambalo limekuwa likijitokeza maeneo mbalimbali nchini ikiwemo wilayani humo.

"Serikali na taasisi mbalimbali ziweze kuwasaidia katika utoaji wa elimu katika jamii ili kuondoa imani na mila potofu ambazo husababisha ukatili kwa wenye ualibino". Alisema Rashid huku akisikitishwa na tukio lililotokea hivi karibuni wilayani Kishapu la mmoja wa wasichana wenye ualibino kutoka Kijiji cha Munze, Kata ya Kishapu kunusurika kubwakwa kutokana na imani potofu.

No comments:

Powered by Blogger.