LIVE STREAM ADS

Header Ads

Milo Clan Watoto wa Mji watikisa Ndondo Cup Jijini Mwanza

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Judith Ferdinand, Mwanza
Timu ya Milo Clan  watoto wa mji, wameilaza chali  wapinzani wao AFC Lumumba goli 2-0,katika mchezo  wa tatu wa hatua ya  robo  fainali mashindano ya ndondo cup,yanayoendelea katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Katika mchezo huo, ambao ulikutanisha timu zote kutoka katikati ya mji,imepelekea Milo Clan kuwa timu ya tatu kufanikiwa kufuzu kuingia hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.
Milo Clan walifunga magoli kupitia washambuliaji wake Sadick Manzicha dakika ya 29 na Daniel Manyenye dakika ya 43.

Mchezaji bora wa mechi hiyo ni Emanuel Swita  wa Milo Clan na kupatiwa kitita cha shilingi 30000, kutoka HASFU Barber Shop.

Naye Kocha  wa AFC Lumumba Hassan Mguda alisema, sababu ya kufungwa ni kutokana na wachezaji wa mbele kutokua makini,japo walicheza vizuri hila bahati haikua upande wao.

Kwa upande wake Kocha wa Milo Fc  Hussein Tade,pia aliomba mashindano hayo yaendelee ili kuendeleza vipaji vya Mwanza kwani yameleta changamoto.

No comments:

Powered by Blogger.