LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwanza Veterans wachuana vikali na Habari Fm Jijini Mwanza

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Judith Ferdinand, Mwanza
Timu ya Mwanza Veterans imetoa kichapo cha goli 7-6, dhidi ya  timu ya wanahabari (Habari FC) ya jijini Mwanza, katika mchezo  wa kirafiki uliorindima  kwenye uwanja wa kisasa na mkongwe wa Nyamagana.

Katika mchezo huo Habari FC ndio ilianza kuona lango la mwenzie baada ya kufunga goli dakika ya  27 kupitia mshambiliaji wake Juma Ayo ambaye pia aliweza kuongeza goli jingine dakika ya 31 na 60, huku magoli mengine yakifungwa na Francis Chamungu dakika ya 39, Dullah Official dakika ya 75 na Mohammed Juma dakika ya 79.

Hata hivyo Mwanza Veterans walifunga magoli kupitia washambuliaji wake Ami Said ambaye alifunga dakika ya 35,38,40 na 45 huku Dadi Phares akifunga dakika ya 59,64 na 81.

Akizungumzia mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Nahodha wa Habari FC Moses Wiliam alisema,wamefungwa kimchezo, na wanakubali matokeo kwa vile walizidiwa uwezo,hivyo wataenda kufanyia kazi makosa yaliyojitokeza,pia aliipongeza Mwanza Veterans kwa kucheza vizuri.

Kwa upande wake Kocha wa Habari FC Baltazar Mashaka alisema, mpira ni mchezo wa makosa,hivyo anaimani mchezo ujao watafanya vizuri  na utakuwa na ushindani, kwani kila mtu amejua nafasi yake,pia aliwaomba waendelee kudumisha ushirikiano ili kukuza soka la Mwanza.

Pia Mashaka alisema, sababu ya timu yake kushindwa ni kutokana na  uzembe wa washambuliaji ambapo wapinzani wao walitumia udhaifu huo na kushinda,licha ya mpira kuwa na matokeo matatu,hivyo wapo katika mpango wa kuhakikisha wanafanya mazoezi ya mara kwa mara ili waweze kufanya vizuri zaidi.

Naye Kocha wa Mwanza Veterans Ibrahim Mlumba,  aliipongeza timu ya Habari FC kwani ni mwanzo, hivyo amepata mchezaji kutoka timu hiyo ambaye atamsajili kwenye kikosi chake  katika ligi daraja la tatu.

Hata hivyo Nahodha wa Mwanza Veterans  Juma Maftah (Pele) alisema mchezo ulikua mzuri, na timu ya Habari FC siyo mbaya ila ikajipange upya katika mchezo mwingine.

No comments:

Powered by Blogger.