LIVE STREAM ADS

Header Ads

Watakiwa kudhani mchezo wa kikapu nchini

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Naibu Waziri Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula kulia akimkabidhi jezi Mratibu wa Mpango wa Mafunzo ya  Watoto ya Mpira wa Kikapu Mwanza Bahati Kizito, katika tamasha la  mpira Wa Kikapu kwa Watoto na Vijana wenye umri chini ya miaka 14 na 16 lililofanyika kwenye uwanja wa mchezo huo Kiloleli

Judith Ferdinand, Mwanza
Wadau mbalimbali nchini wamehimizwa kudhamini mchezo wa kikapu (Basketball), ili kuendeleza na kuhamasisha jamii kuupenda kama ilivyo kwa mpira wa miguu.

Wito huo umetolewa na mmoja wa wachezaji wa mchezo huo wenye umri chini ya miaka 14 Mabula Daniel katika tamasha la Mpira wa Kikapu kwa Watoto na Vijana walio chini ya umri wa miaka 14 na 16, lililofanyika jana kwenye uwanja wa Kiloleli huku Mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mbunge wa Ilemela Angeline Mabula.

Daniel alisema, mchezo huo umekosa mashabiki kutokana na kukosekana kwa wadhamini,sambamba na kuiomba serikali kuwahimiza wazazi kuwaruhusu watoto kujiunga na mchezo huo ili waonyeshe vipaji na kuacha kufanya vitendo vya kihalifu.

Naye  Mratibu wa Mpango wa  Mafunzo ya Watoto ya Mpira wa Kikapu Mwanza Bahati Kizito alisema, kupitia tamasha hilo watachagua wachezaji watakaounda timu ya Mkoa kwa umri tofauti,zitakazoenda kushiriki mashindano yatakayoandaliwa na kituo cha mpira Wa Kikapu cha JMK Park cha jijini  Dar es salaam mwishoni mwa desemba 2017.

Huku wasichana watakaofanya vizuri watachaguliqa kwenda kambi ya timu ya taifa,itakayofanyika mwanzoni mwa desemba 2017 katika shule ya sekondari Orkeeswa iliyopo Monduli mkoani Arusha, na vijana mwakani wanatarajia kwenda kucheza na timu zilizopo nchi za Rwanda,Uganda na Kenya, ikiwa ni njia ya kuendeleza mpira wa Kikapu nchini.

"Mbali na mfanikio tunakabiliwa na changamoto mbele yetu ya kupelekea wachezaji na timu katika mashindano, hivyo tunakuomba mgeni rasmi(Angeline Mabula) utusaidie kuhamasisha makampuni,taaasisi na wadau mbalimbali kujitokeza kudhamini na kufanikisha safari hizo pamoja na mchezo huo," alisema Kizito.

Kwa upande wake Mabula alihaidi kushirikiana na kuunga mkono juhudi za kuibuka vipaji vya mpira wa Kikapu na mchezo mbalimbali hasa katika jimbo lake la Ilemela.

Pia aliomba,tamasha la mpira Wa kikapu kwa watoto na vijana, liwe linafanyika mara kwa Mara mkoani Mwanza, ili iwe chachu kwa watoto wengine kujitokeza kucheza sambamba na makoja kujitokeza kufundisha.

No comments:

Powered by Blogger.