LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ni burudani, mbio za Rock City Marathon 2017 Jijini Mwanza kesho

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Judith Ferdinand, Mwanza
Mbio za Rock City Marathon 2017 zinatarajia kutimua vumbi kesho katika uwanja wa CCM Kirumba, huku  Mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri wa Michezo,Sanaa na Utamaduni Juliana Shonza.

Shonza anatarajia kuwa kivutio katika mbio hizo  ambazo zinafanyika kwa mara ya nane mfululizo mkoani Mwanza,kwani  atashiriki kukimbia mbio za km 5.

Akizungumza na waandishi  jijini hapa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Zenno Ngowi alisema, kamati yake imejiandaa vilivyo na maandalizi yamekamilika ikiwemo kupokea wakimbiaji kutoka nje na ndani ya nchi.

" Tunatarajia viongozi wa  serikali, wadhamini wetu wakiwemo PUMA,Tiper,NSSF,Bodi ya utalii Tanzania na wengine pamoja na watu wenye ulemavu wa  ngozi watashiriki kikamilifu katika mbio za km 5," alisema Ngowi.

Pia akizungumzia barabara zitakazohusisha mbio hizo zitakazoanza saa 12 asubuhi kwa washiriki wa  km 42 na 21 wataanzia CCM Kirumba, km 5 barabara ya Nyerere eneo la polisi Mabatini, km 3 mbio za wazee wataanzia barabara ya Nyerere eneo la makaburi ya wahindi na kwa mbio za watoto za km 2 wataanzia Mwaloni kuelekea uwanjani.

Aidha alisema, kwa upande wa mbio fupi za mita 100,200,400,800 na 1500, ambazo ni mahususi kwa wanafunzi zitafanyika ndani ya uwanja, hivyo aliwaomba  wazazi kuwasaidia watoto kufanikisha.

Kwa upande wake  Mratibu wa mbio hizo kutoka Kampuni ya Capital Plus International Bidan Lugoe alisema, zaidi ya milioni  40 zitatolewa katika mashindano hayo,  kwa pande zote mbili mwanamke na mwanaume huku   mshindi wa kwanza mpaka wa tatu wa km 42 na 21 watapatiwa medali pamoja na pesa taslimu.


Pia alisema, kuna zaidi ya waamuzi 100 wa mbio hizo,ambao watasimamia ili washiriki wasiweze kufanya udanganyifu, pamoja na hali ya ulinzi na usalama ipo vizuri kwani kuna jeshi la polisi wakishirikiana na KK Security.

No comments:

Powered by Blogger.